2017-08-11 16:02:00

Mshikamano kwa ajili ya kusaidia Mfuko wa Sadaka ya Kitume


Ni ishara ya upendo ile ya kuwapokea wakimbizi kutokana na Chama cha watakatifu Petro na Paulo walio hamasisha na kufanya mshikamano wa kusaidia mfuko  wa sadaka ya kitume Vatican kwa njia ya chakula cha hisani. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu  Konrad Krajewski, Mtunza sadaka  wa Vatican anasema sadaka zilizokuswanywa kwa matukio ya mwaka katika michango ya hiari imewezesha kwa namna ya pekee mpango wa wakimbizi. Hiyo ni pamoja na kuwa na familia zilizopata mahali pa kukaa Mjini Vatican kutoka nchi ya Siria wakikimbia vita ikiwa ni njia ya kutoa mshikamano wa Baba Mtakatifu Francisko wakati wa ziara yake ya kitume  katika kambi  ya wakimbizi Kisiwa cha Ugiriki na Lesbos. 

Rais Calvino Gasparini na mwongozi wa kiroho Monsinyo Joseph Murphy walikubali mara moja katika kutoa sadaka. Hii ni kutaka kuonesha wazi mshikamano wa vyombo hivi viviwili ambayo ambavyo kama mkono wa Vatican katika upendo kwenye makambi. Na pia mshikamano ambao Mt. Yohane Paulo II aliuelezea kama kuwani mshikamano wa nyumba ya Papaambao unawakilisha kwa namna moja au nyingine kujitoa kwa imani na huduma ya Baba Mtakatifu. Kwa njia hiyo vyama , familia na marafiki ambao wameunganika kwa pamoja katika chakula cha hisani katika Chuo Cha Mtakatifu  Joseph wamekuwa na nia hiyo.

Matukio kama haya ya chakula cha hisani kwa ajili ya kuhamasisha mshikamano yamekuwa yakitendeka katika vyama katoliki  vya kujitolea mjini Roma kwa ajili ya huduma ya Baba Mtakatifu.Moja ya sehemu tatu za vyama hivyo ilianzishwa  na Mwenye Heri Paulo VI mwaka 1971 ya upendo inajishughulisha kwa hali na mali katika mshikamano  kwa namna ya peke kusimamia kila siku watu wenye kuhitaji, kwa njia ya huduma ya kujitolea mjini Vatican; katika nyumba ya watawa wa Mtakatifu Teresa wa Kalkuta, pia wengine ni madaktari ambao wanawasaidia watawa wa Mtakatifu Vincent wa Paoli katika Kituo cha Afya cha watoto cha  Mtakatifu Marta.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.