2017-08-05 16:37:00

Askofu Jean Noel Diouf ang'atuka madarakani!


Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa na Askofu Jean Noel Diouf wa Jimbo Katoliki Tambacounda, nchini Senegal. Wakati huo huo Baba Mtakatifu amemteua Askofu Jean Pierre Bassène, wa Jimbo Katoliki Kolda, kuwa Msimamizi wa kitume wa Jimbo Katoliki la Tambacounda (Senegal). Itakumbukwa kwamba Askofu Jean Pierre Bassène alizaliwa tarehe 1 Agosti 1951huko Essyl. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi akapewa Daraja takatifu ya Upadre hapo tarehe 11 Aprili 1980. Tarehe 22 Desemba 1999 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Kolda na kuwekwa wakfu kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo hili kunako tarehe 29 Aprili 2000.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.