2017-08-04 14:30:00

Maneno ya Mungu hayapitwi na wakati bali yanatuhusu hata leo!


Tuiombee nchi Takatifu: siyo  mbali na eneo waliokuta  masalia ya Mtakatifu Stefano ambaye ni msimamizi  wa nchi hii; eneo hili ni maarufu  katika kusikitisha maana kuna ukuta wa kutenganisha nchi. Ni utumbuzi muhimu wa wayahudi  na warabu ambao kwa pamoja  wanaitwa kushirikishana huruma ya Mungu mwenye nguvu na uweza pia ulazima wa kujishinda  wenyewe ili  kujenga na kulinda mioyo kwa ajili ya kupata amani ya kweli na yenye kudumu.
Haya ni maneno ya Kardinali Leonardi Sandri Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya makanisa ya Mashariki  Alhamis, tarehe 3 Agosti 2017 wakati wa maadhimisho ya misa ya kipapa katika Sikukuu ya msimamizi Mtakatifu Stefano shahidi kwenye Kanisa Kuu la  Mapatano.

Katika mahubiri yake Kardinali Sandri amesema, Bwana hafichi maajabu yake kwa maana anaweza hata kuwahukumu mitume wake. Ameonesha kwamba maneno hayo katika somo  hayaelezi mambo ya kale  au yaliyopitwa na wakati bali maneno ya Mungu yanaendelea hata leo katika ulimwengu uliojaa machungu kwa namna  ya pekee katika dunia ya  nchi za Mashariki ambamo ndugu na marafiki wanaishi na kuendelea kuteswa. 
Kardinali Sandri akiongelea juu ya ndugu wa Iraq  amekumbuka watu waliokufa akianzia na Askofu Raho wa Mosul, Padre Ragheed Ghanni, hadi mapadre,watoto na waamini  wengine katoka Kanisa kuu  Katoliki  la Mama wa shauri jema huko Baghdad. Katika kutafakari mateso makubwa ya namna hiyo anasema ni vema kuendelea mbele kwa kumtumania Mungu.  Amemalizia mahibiri yake akiomba Mungu  neema ya  kuwa watu  wa matumaini ambao wanaonesha mwanga na kwamba Mungu aimarishe zaidi neema  hiyo ndani ya mioyo yao. Na Mama Maria  mama wa Mungu aliyeona  Jumuiya ya kutume huko Yerusalem ikikua pia  shahidi Mtakatifu Stefano azidi kuwa mfano mwema wa kuigwa.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.