2017-08-02 13:47:00

Maziwa ya mama kwa mtoto katika miezi sita ya kwanza ni uwekezaji


Tathimini mpya iliyotolewa tarehe Mosi Agosti 2017 kwa ushirikiano wa UNICEF, Shirika la Afya duniani (WHO) na mradi mpya wa kimataifa wa unyonyeshaji inaonyesha kuwa hakuna nchi inayokidhi kikamilifu viwango vya unyonyeshaji vilivyokuwa vimependekezwa. Viwango vya unyonyeshaji vilivyofanyiwa tathimini katika nchi 194 vimebaini kwamba asilimi 40 tu ya watoto walio chini ya umri wa miezi sita wananyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kitu kingine na nchi 23 pekee duniani ndizo zenye kiwango cha unyonyeshaji pekee wa zaidi ya asimilia 60.

Kunyonyesha ni mojawapo ya njia muafaka ya  uwekezaji muhimu wa gharama nafuu unao weza kufanywa na taifa lolote katika afya ya kizazi kipya na mustkabali bora wa kiuchumi na jamii. Aidha ambao kila taifa linaweza kufanya kwa ajili ya afya ya watu wake  ambao bado ni vijana , na kwa hali ya uchumi wa kijamii endelevu. Haya yamesemwa na mkurugenzi mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Anthony Lake. Bwana Lake amesema kushindwa kuwekeza katika unyonyeshaji , tunawaangusha kina mama . Naye Dr Tedros mkurugenzi mkuu wa WHO amesema unyonyeshaji unampa mtoto mwanzo mzuri wa maisha, huku maziwa ya mama yakiwa kama chanjo ya kwanza kwa mtoto na pia  kumlinda na maradhi na kumpa lishe bora anayohitaji ili kuishi.

Tathmini hiyo pia imebaini kwamba uwekezaji wa dola 4.70 kwa kila mtoto mchanga unahitajika ili kuongeza kiwango cha unyonyeshaji pekee kwa watoto walio chini ya miezi sita ili kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka 2025 .Kwa njia hiyo wanaweza kuokoa maisha ya watoto 520elfu walio chini ya miaka 5, na kuongezea nguvu ya mapato  ya kiuchumi ya milioni  300 za kimarekani kwa miaka 10, hivyo wanaweza kupunguza magonjwa mengi yanayo wakumba watoto na gharama za bima ya afya. Aidha  utakuta mama na watoto inabidi kulipa gharama mara mbili ambayo ni kupoteza maisha na kupoteza fursa. 
Watoto walio wengi wadogo wanakufa kwasababu ya kukosa uwekezaji juu ya  kunyonya kutoka kwa mama zao. Kwa mfano katika nchi tano  na kati ya hizo ni mataifa makubwa kiuchumi lakini ni yenye dharura kama vile China, India, Indonesia, mexco, Nigeria, kadiri ya watoto 236,000 hawaishi kwa mwaka.

Kwa njia hiyo  Ripoti imeonesha kuwa kunyonyesha ni jambo muhimu na hasa kwa kipindi cha miezi sita ya maisha. Kwasababu inamsaidia mtoto kutokuwa na magonjwa ya kuharisha na ugonjwa wa mapafu , ambayo ni magonjwa makuu yanayosababisha vifo vingi kati ya watoto wachanga. Kunyonyesha kunaleta faida katika ngazi ya utambuzi  hiyo ni  kwa upande wa mama hata kwa wadogo, na pia upunguza hatari ya magonjwa ya saratani ya kizazi na maziwa.

Naye Roberto Bertollini, mwakilishi wa Kamati ya kisayansia na Kamati ya Afya na Mazingira barani Ulaya anathibitisha kuwa, kitendo cha kunyonyesha katika maziwa ya mama ni dhahiri kinawezesha kuzuia magonjwa hayo  na hivyo kupunguza hata gharama zinazohotajika katika afya  pia gharama hizo kuwa ndogo katika jamii. Kwa upande wa familia, inakuwa ni faida kubwa kutokana na kwamba maziwa yasiyo ya mama yanauzwa bei ghari.
Pamoja na hayo maziwa ya mama yana zidisha ukuaji  wa ubongo na hata katika mwendendo wa mtoto, kwa namna hiyo unawafanya  watu kuku na afya nzuri inayopoendeza , hata kunafanya mtoto awe na maendeleo mazuri ya shule na hata katika upande wa kazi.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.