2017-08-01 15:02:00

Wakimbizi zaidi ya 250 elfu warudi katika mji na vijiji vya Ninawi


Waziri wa uhamiaji na uendeshaji wa manbo ya ndani nchini Iraq ameripoti kwamba zaidi ya watu 250 elfu wameweza kurudi katika maeneo yao ya asili katika mkoa wa Ninawi. Watu hawa walikuwa wamendoka katika kanda hiyo kutokana na maeneo hayo kushikiliwa na wanangambo wa kijihadi wa Serikali ya Kiislam (Daesh).Taarifa hizi zilitolewa na mwakilishi wa Waziri wa Iraq  wa wahamiaji  akihojiana na Radio Sattar Nowruz. Mwezi wa sita mwaka huu, Waziri mwenyewe  alikuwa amethibitisha kuwa raia waliosongamana  katika Wilaya za Ninawi  tangu mwaka 2016 walikuwa wanakaribia 820, elfu na kwamba kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi ndani ni sawa na kuongezeka kwa shughuli za kijeshi kwa ajili ya kuikomboa Mosul.

Katika msongamano  mkubwa wa watu kutoka Ninawi wapo hata maelfu ya wakristo tangu Julai na Agosti 2014 ambo waliacha mji wao na vijiji vya milima ya Ninawi dhidi ya vitisho na vurugu za  wanamgambo  wa Kijihadi wa Daesh. Wakimbizi hao waliweza kupata mahali pa kijihifadhi katika maeneo ya Kurdistan nchini Iraq. Na katika mahojiano ya tarehe 28 Julai 2017 Patriak Louis Raphael Sako alikumbuka kwamba kuikomboa Mosul haifuti vitendo vyote vya hatari na uyumbaji uliopo katika kanda hiyo.  Aliongeza kusema kwamba, nyumba nyingi ziliangushwa chini wakati wa vurugu na ghasia za wana jihadi.Kutokana na matendo hayo lazima yazidi kuongeza wasiwasi wa familia nyinyi za kikristo ambazo zinapaswa kurudi katika maeneo yao ya asili ambayo kwa sasa ni magofu sasa.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.