Inahesabika kuwa asilimia 10% ya madawa yanayozunguka katika ulimwengu huu ni bandaia,
hicho ni kiasi yenye kuwa na thamani ya mabilioni 85 za Euro. Taarifa hii imetolewa
na Kituo cha utafiti wa kufuatilia madawa ya bandia mjini Paris Ufaransa . Na Kwa
mujibu wa watafiti hao pia wanasema kwa upande wa Afrika chini ya Jangwa la Sahara
ni asilimia 30% ya madawa ya bandia yanayoingia katika nchi hizo.
Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la kudhibiti madawa mipakani wanasema nchi ya
India ndiyo nchi inayo ongoza ya kwanza kutokea madawa haramu magendo na madawa yaliyofungwa
vibaya au yamekwisha muda wake. Mbele ya matukio haya yanayozidi kuenea na ambayo
nchi zinashindwa kuthibiti baadhi ya wameanza kutafuta ufumbuzi na kuweka katika
matendo.
Mfano mmojawapo ni JokkoSante kutoka nchi ya Senegal ambaye amezindua dhana ya
kunnuua madawa kwa njia ya mtandao, lakini njia hii bado iko katika hatua ya majaribio.
Njia hii inatoa hata mfumo wa kampuni kubwa kutoa madawa bure kwa wale ambao hawawezi
kulipia na hasa nchi ambazo kwa asilimilia 50% ya watu wake hawana bima ya afya.
Njia nyingine pia inaitwa Sproxil ilianzishwa tangu mwaka 2009 ambayo inamsaidia mtu
kuhakikisha ukweli wa dawa anayohitaji na inapotokea kwa njia ya simu na kuhakikisha
ukweli wa wa madawa hayo. Kwa miaka 6 hivi njia ya Sproxil imehasabu sasa zaidi na
milioni 50 ya ujumbe wa simu kutoka Afrika na India.
Mkutano uliofanyika nchini Liberia mwezi Aprili 2017 wa Jumuiya ya Uchumi wa nchi za Afrika ya Mashariki (Cedeao) ilitangaza uzinduzi wa kampeni ya Utafiti kuhusu magendo ya madawa na zile ambazo zimekwisha muda wake au bandia na zaidi ya hayo kampeni ya kuhamasisha. Tatizo la upatikanaji wa madawa , unaathiri hasa sehemu kubwa ya idadi ya watu wenye hali ngumu ambao hawana uwezo wa kununua na pia hawazingatii kutafuta chanzo cha dawa hiyo mahali inapotokea. Taarifa inaonesha pia hali hali ya kwamba , mwaka 2013 katika kutaka kupambana na malaria, dawa za bandia zilisababisha wasababiha vifo vya watoto zaidi ya milioni 122 wa afrika.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |