2017-07-31 14:52:00

Vijana Katoliki Barani Asia kuunganika Jakarta nchini Indonesia


Kuanzia tarehe 30 mwezi wa Saba hadi tarehe 9 Agosti huko Jakarta nchini Indonesia kutakuwa na wiki ya vijana Barani Asia (Asian Youth Day – AYD).
Ni mkutano unaofanyika kila baada ya miaka mitatu. Katika nchini humo mkutano wa kwanza ulifanyika mwaka 1999 kwa vijana wakatoliki wakiwa na mada  isemayo “Furaha ya vijana wa Asia: kuishi Injili barani Asia yenye tamaduni nyingi”. Mkutano huu wa vijana ulikubaliwa na Shirikisho la Mabaraza ya maaskofu Barani Asia (Fabc), kwa sasa utaendesha shughuli zake hizo chini ya usimamizi wa  kitengo cha ofisi ya walei na familia.
Ikumbukwe kuwa taarifa hii ilitolewa tangu mwaka 2014 mara baada ya ziara ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Corea katika kilele  cha maadhimisho ya siku hiyo ya vijana, 30 Julai -2Agosti 2014.

Sherehe hiyo ya vijana imegawanyika katika sehemu tatu ambapo vijana wameanzia kukutanika katika majimbo mbalimbali. Sehemu ya pili ni kuunganika katika mji wa Jacarta kwa ajili ya katekesi, liturjia , na kushirikishana uzoefu  mbalimbali wa maisha yao na vijana wengine ; aidha  kutafanyika mkutano kwaajili ya viongozi wa vijana kichungaji. Na sehemu ya mwisho itakuwa kilele cha Sikukuu hiyo ya Vijana. Ili kuweza kuwashirikisha pia wakazi wa Indonesia juu ya Siku ya vijana kwa mwaka 2017 walifanya marathon ya michezo tarehe 7 Mei 2017 ambayo iliwakusanya watu takribani 5000.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 
All the contents on this site are copyrighted ©.