2017-07-31 15:12:00

Kwa mujibu wa Unicef watoto 850 elfu wamerundikana nchini DRC


Kwa mujibu wa taarifa kutoka Unicef inasema zaidi ya milioni moja ya watu wamelazimika kukimbia makazi yao kutokana na vurugu na ghasia zinazoendelea  katika kanda za Kasai nchini  Jamhuri ya Kidemokarasia ya Congo. Hali hii imefanya maisha kuendelea kuwa magumu na hasa  kwa upande wa watoto walio rundikana katika makambi ya wakimbizi au sehemu za vijijimi mahali ambapo watu wamewapokea na kuwahifadhi. Hayo yamesemwa na Jajudeen Oyewale, mwakilishi wa Unicefu katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Jumla ya watu milioni 1.4 ya watu , na kati yao watoto 850,000 wamerundikana. Watu wengine  walio rundika wako wanaishi na familia au ndugu zao wakati  jumuiya hizo ni  masikini katika nchi hiyo. Baadhi ya wengine waishi katika misitu wakitengeneza vinyumba vya kubahatisha kwa siku. Aidha  matatizo makubwa ya mrundikano huo ni ukosefu wa chakula , maji , mahali pa kulala, madawa, vyoo na huduma nyingi muhimu za maisha ya binadamu.

Pamoja na hayo, Unicef inajaribu kutafuta namna ya kuongeza mipango ya kifedha ili kuwasaidia watu hawa walio rundikana wawapatie nyenzo kiuchumi ili kuweza kukidhi mahitaji yao madogo ya maisha. Hadi sasa  kwa njia ya mpango huo Unicef wameweza kuwasaidia familia 11,225. Pamoja hayo hatua nyingine zinafanyika  ili kuweza kuendeleza mpango huo wa kusaidia kwa njia ya fedha. Mpango uitwao "Rapid Response Mechanism" (Rrn) wameamua kufanya kampeni katika wiki zijazo. Lengo la Mpango wa Kampeni hiyo ni kutafuta vifaa vya afya, lishe , maji , ujenzi  wa vyoo na baadhi ya nyenzo na vifaa ambavyo siyo chakula kama vile vifaa vya ukimbizi ndoo za kuchota maji  na vifaa vya kujifunika kama vile mablanketi na mashuka.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 
All the contents on this site are copyrighted ©.