2017-07-31 14:20:00

Amani bado ni changamoto pevu Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati!


Serikali imeacha kujihusisha na nchi na hivyo makundi  yenye silaha kali wamwkuwa mabwa wa vita wanaotawala kwa mabavu na vitisho, wamekuwa na uamuzi juu ya maisha  na vifo vya watu.Haya ni maneno yaliyosemwa na  Kardinali  Dieudonné Nzapalainga  Askofu Mkuu wa Bangui hivi karibuni. Bado matatizo nchini humo yanaendelea pamoja na kutia sahini za makubaliano ya amani  iliyofanyika Roma tarehe 19 Juni mwaka huu kati ya viongozi wa serikali na wa makundi ya kisiasa yenye msimamo mkali juu silaha. Kwa upande wake anasema suluhisho lipo hasa lile la  kwenda katika vijiji na kubaini yale makundi ya kweli ili kuweza kuonana nao, kuongea nao na kuwaomba wasalimishe silaha hizo katika  kujenga uhusiano kati yao na madaraka ya nchi.

Serikali inahesabu baadhi ya makundi yenye silaha ambao wanatawala biashara ya silaha, dhahabu, almasi na aina nyingine za madini na kulinda baahadhi ya maeneo hayo ya machimbo. Askofu Mkuu anasema hawa ndiyo mabwana wa nchi, maana wamejichukulia kuwa na haki ya maisha na vifo vya watu. Askofu Mkuu anaandika akitoa taarifa ya hali ya nchi yake kwa sasa na kutoa baadhi ya ushauri ambao ungeweza kufanyika  ili kuweza kuleta amani ya kweli katika nchi hiyo.Hivi karibuni mwanamke mmoja mjamzito wa kiislam alitekwa nyara na baadhi ya vijana, wakati huo huo makundi hayo ya kihalifu wakachoma makazi  pia kuwateka nyara pia baadhi ya wahudumu wa Caritas. Jumuiya ya waislam sasa imwekewa ulinzi katika maeneo yao. 

Askofu Mkuu pia nasema, alikuwa katika matembezi ya kitume huko Bangui mahali ambapo makundi haya ya silaha yalikuwa yameshambulia jumuiya hizi. Katika safari hiyo aliongozana na mmojawapi wa Askofu na kuweza kuongea na vijana hao ili waweza kusalimisha silaha hizo. Kwa njia hii iliweza kutuliza kwa kiasi kidogo. Aidha askofu anaeleza ni kitu gani kinatoa msukumo wa makundi haya kuwa ya vurugu,  kwamba makundi haya yamejitwalia madaraka juu ya serikali na kutawala kwa vitisho. Watu hawezezi kwa sasa kwenda katika mashamba wakiwa huru au kwenda kupata matibabu au watoto kwenda mashule.

Tatizo kubwa la makundi yenye silaha ni fedha zitokanazo na kila aina ya madini iliyopo nchini humo. Fedha zote hizo zinaishi katika mikono ya makundi haya yenye silaha badala ya kutumika kujenga mashule au hospitali. Wamekuwa vitisho kwa wananchi kiasi cha kuwafanya watu waishi maisha magumu kupindukia. Viongozi wa vitongoji, kata na wilaya hawana nguvu tena. Kwa mfano utakuta katika mji wa Bangassou kuna walinzi saba wakiwa na sihala 2 tu  na polisi 4 wakiwa na silaha moja tu. Katika wilaya kuna makundi  ya kihalifu yanayo wasimamisha watu na kuwataka fedha. Je ni jinsi gani ya kuwafanya hawa vijana? hakuna, anasema Askofu Nzapalainga. Kwa njia hiyo ingefaa kwenda kwenye vijiji na kubaini viongozi wa kweli wanaongoza makundi haya ya kihalifu ili kuongea nao, kuwaomba wasalimisha silaha zao. Na hii ingesaidia  kujenga uhusiano mzuri wa Serikali ili kurejesha hali ya utulivu na amani.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 
All the contents on this site are copyrighted ©.