Kwa miaka 30 ijayo Afrika itakuwa maradufu ya watu wake. Tafiti katika sekta mbalimbali
zinaonesha kuwa iwapo uzazi utaendelea kama ilivyo katika ngazi ya sasa. Katika
ngazi ya kimataifa ya nchi ambazo zina watoto wengi, katika mfulurizo wa nchi kumi
na tano za kwanza ni kutoka Afrika: zinaonesha kuanzia watoto 6 , 7 kwa kila familia
katika nchi ya Niger, na watoto 6 , 5 katika nchi ya Somalia, 5, 7 katika nchi ya
Nigeria na kuendelea.
Katika mkutano wa G20 huko Hamburg, Rais wa Ufaransa Bwana Macron wakati wa hotuba
yake aliamsha hisia za watu na kuleta utata mwingi katika mkutano huo kwamba mwenendo
wa namna hii unawakilisha matatizo, kwa kuzingatia wakati ujao kwenye mtitiriko wa
wahamiaji ambao wanaingia hata Ulaya.
Profesa mmoja wa Chuo Kikuu Katoliki Milano nchini Italia Bwana Gian Carlo Blangiardo anasema, idadi ya watu huenda kuna tofauti ndogo lakini ni mwenendo wenye kiini cha chini. La msingi ni kujaribu kurejea na kubadilisha hali hii ndiyo mali asili. Ni muhimu kujenga maendeleo na kusaidia Afrika ili kuongeza urithi wake na mali zake msingi za kibinadamu; hiyo anasisistiza, ndiyo wajibu na haki juu ya mpango wa kimaadili lakini pia juu ya mpango wa suala la hali ya uchumi. Pamoja na hayo nchi ya Denimark imekwisha tangaza juu ya kutoa misaada kwa ajili ya kuthibiti uzazi katika nchi zinazoendelea. Kwa mujibu wa Professa Blangiardo , anasema nchi za Ulaya kaskazini wanao msumari uliosimikwa kwa ajili ya siasa za mpango wa familia, na kwamba utafikiri mabaya ya ulimwengu huu yanatokana na hilo. Kwa njia hiyo anasema Denimarka na nchi nyinginezo zinapaswa kutambua kwamba mwenendo wa mpango wa uzazi katika ulimwengu unaoizunguka Afrika tayari una mtazamo wa kwenda taratibu na kuendelea halikadhalika kupungua. Kwa njia hiyo ni kusema kwamba hakuna haja ya kusema watatatua aina ya tatizo hilo maana kwao hiyo inajitokeza taratibu.
Aidha Profesa anasema kuwa, bomu la idadi ya watu ambayo ilikuwa na nia ya kulipuka haitalipuka. Sijuhi nini maslahi ikiwa ni pamoja na uchumi wa Denmark ambao umetaka kufufua uwezo huu mkubwa katika soko la Afrika, uwezekano wa kufagia aina mbalimbali za bidhaa ambazo kwa namna fulani madhumuni yake ni mpango wa uzazi. Afrika tayari inakabiliwa na hali fulani ya kupungikiwa na watoto hali ambayo kwa namna moja wazee ni wachache, pia watoto wachache lakini pia uwepo wa nguvu ya uwezekano wa uzalishaji. Afrika yawezekana ikawa kuwa taifa kubwa kama Marekani kwa Karne ya 21.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |