2017-07-08 15:20:00

Papa Francisko ateuwa Makatibu wakuu wasaidizi Baraza la huduma!


Baba Mtakatifu Francisko amewateua Monsinyo Segundo Tejado Munoz, Padre Nicola Riccardi na Dr. Flaminia Giovanelli kuwa ni Makatibu wakuu wasaidizi wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Endelevu ya Binadamu. Kabla ya uteuzi huu, Monsinyo Segundo Tejado Munoz, alikuwa ni Katibu mkuu msaidizi wa Baraza la Kipapa linaloratibu misaada ya Kanisa Katoliki, Cor Unum, ambalo kwa sasa limevunjwa na kuwa ni sehemu ya Baraza jipa ya Kipapa la Huduma ya Maendeleo Endelevu ya Binadamu!

Baba Mtakatifu amemtea pia Mheshimiwa Padre Nicola Riccardi, O.F.M., Jaalim kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Antonianum kuwa Katibu mkuu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Endelevu ya Binadamu. Kabla ya uteuzi huu alikuwa anafundisha masuala ya haki na amani Chuoni hapo. Mwishoni katika orodha hii, Baba Mtakatifu amemteua  Dr. Flaminia Giovanelli, kuwa Katibu mkuu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Endelevu ya Binadamu. Kabla ya uteuzi huu, Dr. Giovanelli alikuwa Katibu mkuu msaidizi wa Baraza la Kipapa la haki na amani. Viongozi hawa wapya ni sehemu ya mchakato wa mwendelezo wa mageuzi yanayotekelezwa na Baba Mtakatifu Francisko kwenye Sekretarieti kuu ya Vatican ili kuongeza tija, ubora, ufanisi pamoja na ukatoliki wa Kanisa!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
All the contents on this site are copyrighted ©.