2017-07-05 16:24:00

Tanzia: Kardinali Joachim Meisner, Amefariki dunia!


Kardinali Joachim Meisner, Askofu mkuu mstaafu wa Jimbo kuu la Kolon nchini Ujerumani amefariki dunia, Jumatano, tarehe 5 Julai 2017 akiwa na umri wa miaka 83. Alikuwa ni Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Kolon kuanzia mwaka 1988 hadi mwaka 2014 alipong’atuka kutoka madarakani! Itakumbukwa kwamba, alizaliwa tarehe 25 Desemba 1933 huko Breslau, Silesia, Ujerumani eneo ambalo kwa sasa ni Poland. Baada ya masomo na majiundo yake ya kitaalimungu ambako alijipatia shahada ya uzamivu, kunako tarehe 22 Desemba 1962 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Tarehe 17 Machi 1975 akateuliwa na Mwenyeheri Paulo VI kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Vina na Askofu msaidizi Jimbo Katoliki Erfurt, Ujerumani ya Mashariki na kuwekwa wakfu kama Askofu tarehe 17 Mei 1975. Tarehe 22 Aprili 1980, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Askofu tarehe 22 Aprili 1980. Kuanzia mwaka 1982 hadi mwaka 1989 alikuwa ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Berlin. Tarehe 20 Desemba 1988 akateuliwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Kolon nchini Ujerumani hadi alipong’atuka kutoka madarakani tarehe 28 Februari 2014. Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Kardinali tarehe 2 Februari 1983.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican. 
All the contents on this site are copyrighted ©.