2017-07-01 18:36:00

Askofu mkuu Giuseppe Pinto ateuliwa kuwa Balozi wa Vatican Croatia!


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Giuseppe Pinto kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Croatia. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Giuseppe Pinto kuwa Balozi wa Vatican nchini Ufiippini. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Giuseppe Pinto alizaliwa kunako tarehe 26 Mei 1952 huko Noci, nchini Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, kunako tarehe 1 Aprili 1978 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 4 Desemba 2001 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu tarehe 6 Januari 2002.

Taarifa zinaonesha kwamba, tangu wakati huo, ametekeleza dhamana na utume wake kama Balozi wa Vatican huko Senegal, Cape Verde, Mali, Guinea Bissau, Chile na Ufilippini. Tarehe 1 Julai 2017 ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Croatia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.









All the contents on this site are copyrighted ©.