2017-06-15 16:14:00

Tume ya kudumu ya Vatican na Israeli yaridhishwa na maendeleo yake


Tume ya Kudumu kati ya Vatican na Israeli, hivi karibuni imehitimisha kikao chake cha siku moja, kilichofanyika tarehe 13 Juni 2017 kwa kuendelea kujadiliana kuhusu kipengele cha 10ยง 2 ya Msingi wa Makubaliano kati ya Vatican na Serikali ya Israeli wa Mwaka 1993. Mkutano huu umeratibiwa na Monsinyo Antoine Camilleri, Katibu mkuu Msaidizi wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican.

Kwa upande wa Serikali ya Israeli, ujumbe wake, uliongozwa na Bwana Tzachi Hanegbi, Waziri wa Ushirikiano. Wajumbe wameridhishwa na hatuma iliyokwisha kufikiwa katika mchakato wa majadiliano baina na Serikali hizi mbili. Matokeo ya mkutano uliohitimishwa hivi karibuni yanatoa nafasi, mazingira na matumaini ya kuweza kuhitimisha majadiliano haya na hatimaye, kuweka sahihi katika Hati ya Makubaliano. Wajumbe wameridhishwa pia juhudi za ushirikiano zinazotekelezwa na pande hizi mbili, katika utekelezaji wa Makubaliano ya Pamoja ya Mwaka 1997 kuhusiana na Viongozi wa Taasisi zinazotambulika Kisheria.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.