2017-06-10 16:03:00

Ujumbe wa Vatican watembelea Ikulu ya Italia!


Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 10 Juni 2017 ametembelea Ikulu ya Italia na kukutana pamoja na kuzungumza na Rais Sergio Mattarella wa Italia. Ujumbe wa Baba Mtakatifu umeongozwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican. Kardinali Agostino Vallini, aliyekuwa Makamu Askofu mkuu Jimbo kuu la Roma ambaye ameng’atuka hivi karibuni kutoka madarakani! Kardinali Gualtiero Bassetti, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Italia.

Wengine katika msafara huu kwa kuzingatia itifaki ni pamoja na Askofu mkuu Adriano Bernardini, Balozi wa Vatican nchini Italia. Baba Mtakatifu Francisko alipowasili kwenye viwanja vya Ikulu ya Italia, amelakiwa na Rais Sergio Mattarella wa Italia na baadaye kufanya mazingumzo ya faragha kati ya viongozi hawa wawili. Wamebadilishana zawadi kama sehemu ya kumbu kumbu ya tukio hili la kihistoria pamoja na kutambulishana wajumbe waliokuwa kwenye msafara wa pande hizi mbili. Baba Mtakatifu amepata nafasi ya kusali kwa kitambo kidogo kwenye Kikanisa cha “Annunziata” na baadaye wakuu hawa wawili wakatoa hotuba zao. Baadaye, Baba  Mtakatifu Francisko na Rais Sergio Mattarella wa Italia wamekutana na kusalimiana na watoto zaidi ya 200 kutoka katika maeneo yaliyoathirika kwa tetemeko la ardhi!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.