2017-06-02 15:20:00

Rais Raimond Vejonis akutana na Papa Francisko na kuteta naye!


Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa, tarehe 2 Juni 2017 amekutana na kuzungumza na Rais Raimonds Vejonis wa Jamhuri ya Latvia, ambaye baadaye amepata pia fursa ya kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Katika mazungumzo kati ya Baba Mtakatifu na mgeni wake, wamepongeza uhusiano mwema ulipo kati ya Vatican na Latvia sanjari na mchango wa Kanisa Katoliki katika ustawi, maendeleo na mafao ya wengi nchini humo. Baadaye wameweza kujielekeza zaidi katika masuala ya kikanda na kimataifa hasa kuhusiana na huduma na ukarimu kwa wakimbizi na wahamiaji; sanjari na matarajio ya Jumuiya ya Ulaya kwa siku za usoni.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.