Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na Washiriki wa Mkutano wa Vyama vya Ulaya vya familia Katoliki (Facce), ambao pia wanafanya maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa shirikisho hilo. Mkutano wa faragha na Baba Mtakatifu umehusu masuala ya thamani ya familia na changamoto zinazokabiliana nazo kama shirikisho katika Bara la Ulaya. Shirikisho la vyama hivi ni kutoka nchi 14 za Ulaya ambao wanayo nafasi kwenye Baraza la umoja wa nchi za Ulaya kwenye mikutano ya Kimataifa vilevile wanayo katiba ya msingi wa haki katika baraza hilo.
Maadhimisho hayo na mkutano wao mwaka kwa siku tatu umegawanyika katika sehemu tatu za tafakari ambapo pia wameweza kuwa na fursa ya kukutana na Baba Mtakatifu tarehe 1 Juni 2017. Shirikisho la vyama hivi katika hotuba yao, pia wameonesha shukrani nyingi kwa Baba Mtakatifu kutokana na Wosia wake kuhusu “Upendo wa furaha”, na Hati ya “Sifa iwe kwako”. Tarehe 31 Mei 2017 washiriki hawa wa Shirikisho la vyama Katoliki Ulaya waliudhuria misa takatifu na kujikabidhi katika kwake Maria ikiwa Kanisa Katoliki linaadhimisha sikukuu ya Mama Maria kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu Roma.
Naye Baba Mtakatifu katika hotuba yake ameanza na shukrani kwa familia zote zinazoundwa Shirikisho la vyama hivyo , wakiwa wakiwa katika maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwake na kumshukuru Rais wa Shirikisho hilo Bwana Antoine Renard kwa maneno ya hotuba yake aliyotoa. Miaka 20 ni michache katika kufanya kazi lakini kwa hakika ni kipindi cha kumshukuru Bwana katika maisha na hamu kubwa ya kupeleka mbele wajibu wenu kila siku mnaojikta nao Baba Mtakatifu amesema. Hali halisi ya shirikisho kijana katika roho na katika historia, inaalikwa kuambukiza hata huduma nyingine za familia ili Ulaya iendelee kuwa na tunu msingi wa familia. Picha ya tunundiyo ilikuwa kauli mbiu ya kuwakilisha mkutano wao wa familia mjini Roma kutoka pande za Ulaya. Baba Mtakatifu anasema. Ni mfano ambao unatafakarisha vizuri na kushuhudiwa na wengi katika familia
Kwa hakika familia siyo vipande vipande vya kuweka katika jumba la makubusho, kwa
kwake familia inathibitisha zawadi, inajikita katika umoja au kuwa wazi katika kupokea
watoto kwa ukarimu na kama ilivyo tabia ya familia inatoa huduma za kijamii. Kwa
maana hiyo familia inakuwa kama chachu inayofanya kukua ulimwengu wa kibinadamu na
kindugu na ni mahali ambapo hakuna yoyote anayejisikia kubaguliwa au kuachwa pweke.
Baba Mtakatifu anasema, shughli zao nyingi zinajieleza katika huduma kamili katika
familia, ambayo ni sehemu msingi wa jamii na ni kama walivyokubaliana hivi karibuni
viongozi wa Umoja wa Ulaya wakati wa tukio la kuadhimisha miaka 60 ya Mkataba wa
Roma. Kazi katika sekta ya Kanisa, ikiwa pia sekta ya kijamii inaweza kuonekana kwa
upesi kwamba ni kujibu mahitaji ya haraka katika mahangaiko tofauti. Lakini hali
halisi kazi hiyo inatoa jibu katika huduma ya habari njema ambayo ni familia.
Akibainisha juu ya wosia wake anasema, Baba katika Wosia wa kitume Furaha ya Upendo ndani ya familia alitaka kuonesha jinsi gani inawezakana kufanya zawadi kwa dhati ikawa njia ya nzuri na ya furaha ya upendo wao kwa wao. Kwa mantiki hiyo, wajibu mkuu unaweza kuwa ni ule wa kuwakumbusha wote kwamba hakuna njia nzuri zaidi ya maendeleo kamili ya jamaii ambayo inalenga kuhamasisha uwepo wa familia katika mfumo wa kijami. Hata hivyo Baba Mtakatifu anabainisha kuwa hata sasa familia inabaki kuwa msingi wa jamii na kuendelea katika ujenzi halisi kwa ajili ya wema wa watu na mahitaji ya kishirikisha kwa ajili ya maendeleo ya kudumu.Halikadhalika katika Wosia huo alitaka kuonesha jinsi gani umoja wao wa wote ndani ya familia na juhudi za mshikamano na jamii nzima ni kwaajili ya kujikita katika wema wa wote na amani hata Ulaya.
Familia ni mahusiano ya kwanza binafsi, ikiwa kwamba ni muungano wa watu. Muungano wa ndoa, ubaba , umama watoto na undugu vinawezesha kila mmoja kujieleza ndani ya familia ya kibinadamu. Namna ya kuishi haya mahusiano yanahitaji umoja ambao ndiyo injini ya kweli ya ubinadamu na uinjilishaji. Kwa njia hiyo leo hii hata daima inaonesha ulazima wa utamaduni wa makutano ambao unatoa thamani ya umoja dhidi ya utofauti, ushirikiswaji na mshikamano kwa vizazi vipya. Huo ndiyo ukuu wa familia unao alikwa kujikita katika mahusiano ya kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa Bara la Ulaya. Mtindo wa familia unaojaribu kuhamasisha siyo kitu cha itikadi za kikundi cha jamii nyingine, bali inahusiana na kutokiuka hadhi na heshima ya binadamu. Hiyo ndiyo msingi wa heshima ambayo Ulaya inaweza hakika kuwa familia ya watu.
Vipeo vya aina nyingi vinachanua kwa sasa katika Bara la Ulaya ikiwa ni pamoja
na hali ya familia. Lakini vipeo hivyo vinachangamotisha kuweza kufanya kazi zaidi
na vema kwa imani na matumaiani, Baba Mtakatifu anaeleza. Baba Mtakatifu anasema kwamba
anatambua mipango yao ya kuhamasisha siasa halisi kwa ajili ya familia katika sekta
ya uchumi na ajira, siyo hiyo tu bali hata inayo jikita katika kutafuta kazi yenye
hadhi kwa ajili ya wote hasa vijana wengi katika kanda za Ulaya wanaoteseka na janga
hili la ukosfu wa ajira.
Katika mipango hiyo na mingine zaidi inayoongozwa na sekta hiyo ya utawala, lazima
iweke kipaumbele zaidi cha kuheshimu hadhi ya kila mtu. Kwa maana nyingine katokana
na tamaduni ya makutano daima kuna haja ya majadiliano ambayo ni muhimu katika kusiliza.
Mazungumzo yenu daima yahusiane na matendo, ushuhuda, uzoefu na namna ya kuishi, kwamba
maisha ndiyo yatoe mifano. Na ndiyo maana ya kipaumbele cha mpango wa Mtangulizi
wake Mtakatifu Yohane Paulo II aliokuwa akiiita Familia.
Aidha amebainisha changamoto za vipeo hivyo kwamba, vipeo vinne vinaikumba Bara la Ulaya kwa muda huu: kama vile upungufu wa idadi ya watu, wahamiaji , ajira na elimu. Kipeo hicho lakini kinaweza kupata upeo chanya katika utamaduni wa makutano, mahali ambao wadau wa kijamii, kiuchumi na kisiasa wanaweza kuungana pamoja na kutoa majibu kulingana na kipimo cha familia, wakitambua vema kwamba familia ni rasiliamali, na ni mkataba wa mtu na mazingira yake. Kwa maana hiyo, kazi ya Shirikisho la Vyama vya Kifamilia mara nyingi wanakutana na majadiliano ya kujenga na wadau mbalimbali wa kijamii, lakini wao bila kuficha kamwe utambulisho wao wa kikristo. Na utambulisho huo Baba Mtakatifu anasisitiza utawafanya kutazama daima upeo wa wazi na kwa umbali. Hiyo ni kama vile wao walivyosema katika hotuba yao kwamba utamaduni wa mbali, unawaalika katika elimu kwa ajili ya kesho.
Ili kweza kujikita katika kazi ya familia ili isibaki katika upweke, inahitaji kujinasua katika upweke huo, inahitaji kuzungumza na kukutana na wengine, ili kutoa mahusiano katika umoja ambao yanakwenda sambamba na maendeleo yoyote kwa manufaa ya pamoja. Baba Mtakatifu anaendelea, familia zimerithi mengi kutoka kwa mababu zao.Wao ni kumbu kumbu ya kudumu ambayo iwasukume ili waweze kuwa na moyo wa hekima na siyo wa teknolojia ya kuunda mipango juu ya familia na kwa ajili ya familia. Wao ni kumbu kumbu; ambapo vijana wa kizazi hiki wanalo jukumu la kutambua kwamba maisha yanaendelea mbele. Kwa mfano wa hekima hiyo katika huduma ya utakatifu wa maisha inakamilika katika ya kizazi. Inakamilia katika kutoa huduma kwa wote, zaidi wenye kuwa na mahitaji, walemavu na yatima. Inakamilika katika mshikamano juu ya wahamiaji, inakamilika katika uvumilivi wa sanaa ya kuelimisha na kuona kwamba kila kijana anahitaji hadhi ya upendo wa familia. Inakamilika katika haki ya maisha na kupokea wale ambao hawana sauti, na inakamilika katika hali ya maisha yenye adhi kwa wazee.
Kazi ya kufanya ni kubwa na nguvu: hivyo Baba Mtakatifu anaongeza kusema, ni kwa njia ya kujibidisha katika vyama vyao , wakiwaalika familia nyingine kujiunga na kazi hiyo inaweza kuwa njia rahisi, kwasababu umoja ni nguvu. Wao wanahitaji wawe chachu inayofundisha wengine kufanya kazi pamoja wakiheshimu tofauti na hali halisi kwa ujumla. Na mwisho amemalizia akiwatia moyo waendelee kuwa wabinifu kwa njia mpya na rasilimali ili familia ziweze kufanya zoezi katika nyanja ya Kanisa kama vile katika jamii kwa kujikita katika aina tatu za shughuli kwa kusaidia kizazi kipya, kuwasindikiza katika kwenye hatua za maisha ambazo mara nyingi kuna ajali za na kuwaongoza ili kuwaonesha thamani na maana ya kutembea kwa pamoja kila siku. Utume huo unaweza kuwa mchango mkubwa wa Shirikisho la Vyama Katoliki vya Familia ameongeza, ni katika shughuli zao za kila siku kwa ajili ya familia za Ulaya. Amewabariki na kuomba sala kwa ajili yake kama kawaida.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |