2017-05-31 17:33:00

Papa awahimiza maaskofu wa Albania umoja na utume wa familia


Baba Mtakatifu francisko Jumanne 30 Mei 2017 amewapokea na kuzungumza na Maaskofu wa Albania ambao wako kwenye hija ya kitume,katika mkutano wao wameonesha matumaini kwako ya Kanisa dogo la nchi hiyo. Katika moyoni mwa Papa Kanisa la Albania linayo nafasi  maalumu kwasababu ni Kanisa lililotesaka sana: kwa miaka 50  chini ya udikteta wa kikomunisti ambao ulitafuta kwa namna moja au nyingine kufuta Kanisa hilo lakini ikashindikana,hata hivyo  ziara ya Baba Mtakatifu  haitasahulika ya kutembelea nchi hiyo mwezi Septemba 2014.
 Katika ziara yake hiyo aliwaalika waamini wa Kanisa Katoliki waruke  kama tai ambayo ni ishara iliyoko katika  bendera ya taifa , lakini pia wasisahau kiota cha ndege huyo ikiwa na maana ya kutosahau mateso ya mashahidi wa nchi hiyo. Kwa njia hiyo mwezi Novemba mwaka jana mashahidi 38 walitangazwa kuwa wenye heri. Hata hivyo katika mazungumzo nao Baba Mtakatifu Francisko amesisitizia kuiga mfano wa mashahidi  hao wa Injili waliolipa nafsi yao kwa ajili kutetea imani yao katika  Kristo.

 Ili kuelezea Mkutano wa maaskofu wa Albania na Baba Mtakatifu,  Askofu Mkuu wa Scutati Angelo Massafra  na Rais wa Baraza la Maaskofu amesema, imekuwa uzoefu mzuri  wa kukaa na Baba Mtakatifu wakijadiliana kwa pamoja katika kupewa nafasi ya kuongea nao bila haraka kwa utulivu,na kwamba kweli wamejisikia kupokelewa vizuri utafikiri walikuwa nyumbani kwao. Askofu amaeleza jinis walivyozungumza  kuhusu kukua kwa Kanisa lao japokuwa ni maskini na shahidi ambapo Baba Mtakatifu amewashauri waendelee mbele  kwasababu Kristo amefufuka na wao ndiyo wako mstari wa mbele kutangaza hilo. Aidha amewaalika kuhamasha miito akisisitiza kuwa shughuli za kichungaji dama zijikite hawali ya yote kupitia ushuhuda. Zaidi amewashauri wawe na umoja katika yao na kuwa na utulivu pia furaha kwasababu ya utambuzi kwamba mwenye furaha ugeuka kuwa mfano kwa wengine.

Alikadhalika wamegusia juu ya majadiliano ya kidini , ambapo wamemweleza juu ya wiki iliyopita kuweka  makubaliano kati ya nguvu za serikali na wapinzani wake: kama wajibu wa Kanisa kwa umma wameweka nao mkataba wa pamoja kati yadini tofauti yaani wakatoliki, waorthodox ,Waluteri , waislam na, bektashi mkataba huo wa pamoja ni wa kupinga machafuko na vurugu , ili kukaribisha ushirikiano, mshikamano na majadiliano.
Ni Mkataba  wa umoja wa Baraza la kidini ambapo Baba Mtakatifu Francisko amefurahishwa juu ya hilo. Amwewashukuru maaskofu kwa mchango wao kwani umewawezesha  nguvu za kisiasa kuwa na makubaliano ambayo wameamua kupeleka mbele tarehe za uchaguzi mkuu ili kuwezesha  wote waweze kushiriki. Kwa njia hiyo askofu anasema hilo ni  tunda la nguvu za Kanisa katika shughuli za majadiliano ya kidini na kiekumene.

Matarajio ya Kanisa la Albania baada ya Mkutano na Baba Mtakatifu Askofu Mkuu Angelo anasema ni kwenda na kutoa ujumbe msingi ambao baba Mtakatifu amewahimiza yaani wa kuwa na umoja kati yao,kujibidisha katika utume wa wafamilia na maskini. Anaongeza kwamba katika Kanisa la Albania walikuwa tayari wanapeleka mbele shughuli za wafungwa na familia zenye waleamavu.Kwa njia hiyo maneno ya Baba Mtakatifu yanatoa msukumo zaidi na kuwaalika jamii nzima ya Albania kuwa na matumani, pia kusali na kuabudu Yesu wa Ekaristi , maana kwa njia ya Kristo tunaweza kwenda katika upeo endelevu anasema Askofu Mkuu Massafra na pia anabainisha kuwa,Papa amewatia moyo na kuwabariki.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.