2017-05-30 15:18:00

Maadhimisho ya miaka 40 ya Upadre wa Askofu wa kwanza wa Finland.


Sikukuu ya kiemkumene katika maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwake  na  miaka  40 ya upadre wa Askofu Teemu Sippo nchini  Finland. Habari hizi zimetolewa na mtandao wa Baraza la Kiekumene la Makanisa ya Finlandia.Habari zinasema kuwa  wakati wa maadhimisho ya Ibada ya misa Jumamosi 27 Mi 2017 katika Kanisa la Mtakatifu Yohane Mbatizaji waliundhuriwa sherehe hizo  wawakilishi wa kiekumene maaskofu wa kiluteri, Askofu Mkuu wa Kiorthodox Leo , Katibu Mkuu wa Baraza la Kiekumene  nchini Finlad na wengine wengi , wadau wanaojikita katika kuhamasiha uekumeni wa madhehebu.

Baada ya Ibada ya misa , ilikuwa  i wakati wa sikukuu ambapo wote walipata fursa ya kumsalimia na kumpongeza Askofu  Sippo ambaye anajikita katikauhamasisha njia ya uekumeni,aidha katika maisha yake ya kitume katika Kanisa la Finlad amejihusisha sana kuudhuria mikutano ya kiekumeni ambapo pia alipata fursa ya kuoongoza kama Rais wa Baraza la kiekumeni kuanzia mwaka 2010 hadi 2015.

Askofu Teemu Sippo alizaliwa katika familia ya kiluteri mwaka 1974 ,ambapo aliweza kuingia katika Kanisa Katoliki akiwa na miaka 19.Akiwa na miaka 23 alifunga nadhiri zake za milele  katika Shirika la watawa wa kime Wadehoniani. Alitangazwa kuwa Askofu  wa Helsink na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI mwaka 2009. Alikuwa askofu Katoliki wa kwanza wa Kanisa mahalia la Finland  tangu kipindi chote cha mageuzi. Idadi ya Wakatoliki kwa sasa nchini Finland ni 15,000 ambapo asilimia 10% ni wahamiaji.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.