2017-05-29 10:37:00

Papa:Bwana awapokee marehemu katika mwanga na kuongoa mioyo ya magaidi


Mara baada ya mahubiri yake na sala ya Malkia wa Mbingu, Baba Mtakatifu Francisko amekumbuka kwa masikitiko makubwa mashambulizi ya hivi karibuni ya kigaidi, na kusema Bwana aweze kuleta uongofu wa  mioyo ya magaidi,pia kuonesha ukaribu wake kwa Kanisa la Kiorthodox nchini Misri walioshambuliwa na magaidi. Amewakumbuka pia waathirika wa Manchester katika shambulio la Jumatatu iliyopita.

Baba Mtakatifu Francisko Jumapili 28 Mei 2017 ameonesha kweli huzuni kubwa na kusema;uchungu mkubwa kwa ajili ya mashambulizi kigaidi dhidi ya waamini wa Kiorthodox waliowawa wakiwa wanakwenda kwenye hija. Ameonesha ukaribu wake wa Mkuu wa Kanisa la Kiorthodox Tawadrso, waamni wake na taifa kwa ujumla. Anasema waamini hawa wakiwemo pia watoto walikuwa wanakwenda hija katika madhabahu kusali , wameuwawa kwa ajili ya kutetea imani yao katika Kristo. Bwana awapokee katika amani mashuhuda wajasiri na mashaidi, wakati huo huo, Bwana aweze pia kuongoa roho za magaidi hao.

Halikadhalika Baba Mtakatifu Francisko ameomba waamini wote waungane naye kusali kwa ajili ya waathirika kutokana na mashabulizi ya kikatili yaliyofanyika Jumatatu iliyopita  huko Manchester Uingereza,anssema vijana wengi wamepoteza maisha yao. Baba Mtakatifu anaonesha ukaribu wake wa sala kwa familia zao na wote wanao omboleza kwa ajili ya kuondokewa na ndugu zao au marafiki.

Baba Mtakatifu amekumbusha tukio la  Siku ya Mawasiliano ya Kijamii duniani kwa mwaka 2017  yanayoongozwa na kauli mbiu “Usiogope maana mimi niko nawe (Is 43,5).Anasema kwamba, vyombo vya mawasiliano vinatoa uwezekano wa kushirikisha na kusambaza habari za wakati huo huo kwa njia moja, habari hizi lakini zinawezekana  kuwa nzuri au ambaya, za kweli au zenye uongo; hivyo anasema tusali kwa ajili ya kila aina ya habari inayotolewa ili iwe yenye ujenz kwa  kutoa huduma ya maisha ya kweli, na kukataa ubaya na uzushi, kwa njia hiyo inaweza kutoa matumaini na uaminifu katika nyakati zetu.

Baba Mtakatifu Francisko amemalizia na shukrani kubwa kwa Kanisa Kuu la Genova, kutokana na makaribisho makubwa aliyopokea kwenye ziara yake ya kitume aliyoifanya  Jumamosi 27 mei 2017. Amewatakia baraka za Mungu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.