2017-05-29 16:16:00

Baba Mt.Francisko amekutana na Waziri Mkuu wa Canada Bw.J.Trudeau


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu , tarehe 29 Mei 2017 amekutana na kuzungumza na Waziri mkuu wa Canada Bwana Justin Trudeau ambaye baadaye pia amekutana  na kuzungumza  na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyeambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican. Mazungumzo yao yameonesha uhusiano mzuri kati ya Vatican na nchi ya Canada na pia mchango wa Kanisa  Katoliki katika maisha ya jamii watu wa nchi hiyo. Baadaye wamezungumzia mada ya ushirikishwaji na mapatano, kama vile juu ya uhuru wa kidini ambayo ndiyo masuala ya sasa ya kimaadili yenye matatizo.

Mwisho amegusia mambo mengine hasa kwa kuzingatia matokeo ya mkutano wa wakuu wa G7 uliomalizika hivi karibuni nchini Italia,na kutazama baadhi ya masuala ya kimataifa,zaidi wakiweka kipaumbele kwa  nchi za Mashariki ya Kati na maeneo yenye migogoro.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.