Afya siyo bidhaa ya kutumia,bali ni haki ya kila mtu na kwamba kupata huduma za afya isiwe kwa upendeleo, pamoja na majengo zenye nguvu na mifumo ya afya ni lazima kuweka kipaumbele cha maisha ya mwanadamu na mahitaji yake kimwili, kidhamiri na kiroho,vilevile kupata matibabu katika kuheshimu zaidi utakatifu wa maisha ya binadamu katika hatua zake zote ikiwa ni pamoja na kutunza hadhi ya kila mtu. Ni baadhi ya mambo muhimu yenye nguvu juu ya afya ya maisha ya binadamu katika hotuba iliyotolewa na Askofu Mkuu Ivan Jurkovič, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican Katika Umoja wa Mataifa kwenye Mkutano wa 70 wa dunia kuhusu Afya ambao umeanza tarehe 22 hadi 27 Mei 2017 huko Geneva Uswiss.
Mwakilishi wa Vaticana anatambua uhamasishaji wa Afya ambao unahitaji kuheshimiwa
na msingi wa mkataba wa agenda 2030 kuhusu maendeleo endelevu ambapo pia unawakilisha
zaidi mambo muhimu kwa ajili ya kuimarisha uchumi jamii. Askofu Ivan anabainisha
kwamba mifumo ya afya inazidi kudorora, pia kuwa kizingiti kikubwa katika nchi nyingi
,matokeo yake ni ukosefu wa bima na huduma msingi za afya.
Changamoto za sasa na za haraka duniani anasisitiza; ni kwa upande wa afya ambapo
inatakiwa mifumo ya afya iliyo bora, yenye uwezo wa kutoa huduma inayofaa na inayopatikana
kwa ajili ya kuzuia na kutibu wote, kwa namna ya pekee kwa watu wanye kuhitaji ,kama
vile maskini wanaoendelea kuongezeka katika jamii, waliobaguliwa, wahamiaji , wakimbizi
ambao kwa sasa wanawakilisha katika jamii wasiwasi na ishara za nyakati hizi. Kwa
mujibu wa Askofu Mkuu Ivan anasema haitakiwi na hakina mtu wa kusahaulika.
Kama alivyoeleza Baba Mtakatifu Francisko kwamba kipimo na rahisi zaidi cha utendaji wa kuweza kufikia malengo ya agenda ya maendeleo endelevu iwapo yataanza kujikita katika vitendo mara moja , kwa watu wote na kwa ajili ya manufaa ya wote kiroho na kimwili inavyotakiwa . Mifumo ya afya yenye nguvu na kweli ni ufunguo wa kufikia melengo endelevu ambayo zaidi ni kuhakikisha maisha na afya na kukuza ustawi wa kila mtu na kwa kila rika la maisha ya binadamu. Juhudi zinazofanywa katika ngazi ya kitaifa kwa kujenga mifumo ya afya bora kwa hakika zinahitaji mwendelezo wa uongozi kiufundi kutoka Shirika la Afya Duniani, pamoja na kuunga mkono na wadahu wa washirika ya maendeleo ili kuondokana na ukosefu wa rasilimali za kifedha katika sekta ya afya. Aidha, pamoja na miundombinu na imara ya kuaminika, mifumo ya afya ni lazima kuweka mbele utu wa binadamu na mahitaji yake kimwili, kidhamiri na kiroho, utoaji wa huduma bora katika kituo,kwa kuheshimu utakatifu wa maisha ya binadamu katika hatua zake zote na hadhi ya kila mtu.
Halikadhalika Askofu Mkuu Ivan anasema; kama mataifa yatajizatiti katika kujenga , kuwekeza na kutekeleza hatua za kukuza maendeleo na miundo mbinu katika ujenzi wa mifumo ya afya inayotakiwa, ni muhimu kwamba, serikali wasizingatie utaratibu mmoja tu wa kusimamiwa na taasisi za serikali, bali wakumbuke kuwahusisha kuanzia wadau wakuu , hasa mashirika ya dini ambayo hutoa mchango mkubwa katika utoaji wa huduma za afya muhimu kwa watu . Aidha anathibitisha kwamba kwa dhati katika nchi nyingi, kuna mashirika mengi ya dini na taasisi nyingine za kidini na zisizo za kiserikali ambazo wanachukua wajibu muhimu kwa ajili ya mifumo ya afya na hivyo wanapaswa kujumuishwa katika uundaji wa sera za afya kisias. Lazima kuwa na upatikanaji wa rasilimali za kutosha ili kuhakikisha nguvu na uwezo wa shughuli hizo katika sekta ya kidini na mashirika yasiyo ya kiserikali zinapatikana.
Askofu anaendelea kueleza ; Mifumo ya afya inayofanya kazi vizuri, ni lazima iwe
na mambo mengine muhimu na hasa maji ya kuaminika, madawa na teknolojia. Hata hivyo,
hali halisi, kama ilivyojitokeza katika ripoti ya Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa
kuhusu maendeleo katika utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo 2030 ya Maendeleo Endelevu,
kuhusiana na upatikanaji wa madawa muhimu ya kuchaguliwa, inahitaji hatua za maamuzi
kwa upande wa jumuiya ya kimataifa. Hiyo ni kwasababu imenukuliwa kwamba upatikanaji
wa wastani wa madawa muhimu yaliyochaguliwa ni asilimia 56% tu katika sekta ya umma
kwa nchi zenye kipato cha kati. Aidha bidhaa mpya bado ziko mbali zaidi kufikia mahitaji
ya afya ya watu wanaoishi katika nchi zinazoendelea.
Na kiasi cha asilimia 1% tu ya fedha zote kwa ajili ya utafiti na maendeleo ya afya
ni lengo kwa ajili ya magonjwa yanayoathiri nchi zinazoendelea. Kwa njia hiyo Askofu
anatoa ushauri kwamba, ni lazima kuanzisha ushirikiano ambao unawezesha kuwa na mwendelezo
wa wa utafiti na maendeleo katika sekta ya afya ambayo ndiyo inahitajika na mahitaji
ya ya afya yeyewe ,hatimaye kuhakikisha idadi kubwa ya dawa muhimu inawafikia wote.
Askofu Mkuu Ivan anamalizia akisema; kama Papa Francisko alivyosisitiza kwamba ,"Afya, kiukweli, siyo bidhaa, bali ni haki kwa watu wote na kwamba kupata huduma za afya isiwe kwa upendeleo . Kwa hali hiyo Baraza jipya la Kipapa kwa ajili ya huduma ya mandeleo ya watu inaaandaa Mkutano wa Kimataifa kuhusu mada ya” kukabiliana na tofauti kimataifa katika afya", ambayo itafanyika katika mjini Vatican kuanzia tarehe 16-18, Novemba 2017. Askofu Mkuu anawaalika kwamba;kuushiriki kwao itakuwa ni mwafaka !
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |