2017-05-25 14:49:00

Mkurugenzi Mkuu mpya wa WHO Dk Tedros Ghebreyesus kutoka Ethiopia


Shirika la Chakula Dunia WHO limemechagua Mkurugenzi Mkuu mpya wa Shirika hilo  Dkt. Tedros Ghebreyesus kutoka nchi ya Ethiopia ambaye anashika nafasi hiyo kwa muda wa miaka mitano. Uchaguzi umefanyika tarehe 23 Mei 2017  kwenye makao Makuu ya Shirika hilo huko Geneva Uswiss ambapo Ghebreyesus alipata ushindi kati ya wenzake wawili David Nabarro wa Uingereza na Sania Nishtar wa Pakistan.
Daktari Ghebreyesus ambaye ni mwafrika wa kwanza kushika wadhifa huo, amechukua nafasi hiyo kutoka kwa Dkt. Margaret Chan ambaye amemaliza muda wake baada ya kuhudumia kwa awamu mbili za kipindi cha miaka mitano mitano. Uchaguzi wa Mkurugenzi huyo umefanyika ndani ya Mkutano wa 70  wa Afya Duniani huko Geneva ulioanza tarehe 22 na utamalizika tarehe 27 Mei 2017.

Mkurugenzi mpya wa Shirika la Afya duniani Dkt Tedros amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uwaziri katika nchi yake ikiwa ni pamoja na nfasi ya Waziri wa Afya wa nchi. Wakati wa kutoa hotuba yake, ameahidi kufanikisha lengo la afya kwa wote kwamba; sasa, ni nusu tu ya wakazi wa dunia wanaopata huduma ya afya bila kikwazo, hivyo hiyo ni lazima kuboreshwa haraka.Na  muda mfupi baada ya kutangazwa kwake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw.António  Guterres amempongeza akisema, ushindi wake utakuwa muhimu katika kuhakikisha maisha yenye afya na kukuza ustawi kwa wote  na kwa umri wote.

Aidha mkurugenzi mpya wa  WHO akizungumza na waandishi wa habari Jumatano 24 Mei 2017  mjini Geneva Uswis anahimisza nchi wanachama kutoa huduma ya afya kwa wote na kutekeleza sheria na mikataba ya kimataifa ya afya . Aidha akielezea masuala ambayo niyakupewa kipaumbele Dkt Tedros amesema sababu ya kuanzishwa WHO 1948  hata leo hii lengo lake bado lina uzito uleule na kwamba,ahadi zilizotolewa wakati ule na Shirika la Afya duniani lazima kuendeleza ari hiyo pamoja na kwamba ni nusu ya watu duniani wanaopata huduma za afya.Ameongeza kusema kwamba anadhani umewadia wakati mwafaka wa kutimiza kauli hizo, hata hivyo dunia nzima inatakwa wajibu huo kwamba afya ni suala la haki.

Mambo mengine ambayo yanatakiwa kupewa kipaumbele: ni jinsi WHO itakavyoshughulikia dharura za kiafya, kuleta mabadiliko na pia kurejesha imani ya wanachama kwa shirika hilo na kuhakikisha michango yao inatumika ipasavyo.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.