Maeneo ya Makundi ya Kiislam Maute yanayojitangaza kuwa na mahusiano na serikali ya Kiislam , walivamia Kanisa Kuu Katoliki la mji wa Marawi nchini Ufilippini na kuwateka nyara waamini karibu 15 kati yao akiwemo Padri mmoja watawa na walei ambao walikuwa wanasali. Ni taarifa zilizothibitishwa na Askofu Mkuu Edwin De la Pena Mwakilishi wa Kitume katika Mji wa Marawi kwenye kisiwa cha Mindanao Kusini mwa nchi ya Ufilipini. Lilikuwa ni kundi karibu la magaidi 100 wa Maute walioshambulia mji huu ambapo Rais wa Ufilippini Bw. Rodrigo Durterte ameagiza mji kulindwa na sheria ya kijeshi katika kisiwa hivho.
Habari kutoka katika gazeti Katoliki la Fides zinasema, Askofu anasema kuwa tarehe 24 Mei 2017 ni sikukuu ya Mama Maria msaada wa Wakristo hivyo waamini walikuwa Kanisani wakisali siku ya mwisho ya Novena kabla ya sikukuu. Magaidi walingia kwa nguvu Kanisani na kuwateka nyara watu ambapo wamewapeleka sehemu isiyojulikana. Kwanza waliingilia nyumba ya Askofu na kumteka nyara Katibu Msaidizi wa Askofu, Padri Teresito Soganub. Na baadaye kuchoma moto Kanisa Kuu ambalao limaharibika.
Magaidi hawa walishambulia mji na kuwaogopesha watu ambapo nyumba zimefungwa wakiwa
wanasubiri wanajeshi anasema askofu. Aidha Askofu Mkuu anasema ili kutuliza nchi hii
damu ni kama kwamba itamwagika kwani kwa upande wa watekwa nyara hakuna habari yoyote
ambayo imeshapatika, japokuwa mchakato umeanzishwa kati ya Kanisa na viongozi wa kiislam;
ni matumaini ya kwamba mchakato unaweza kusaidia ili watu waliotekwa nyara waweze
kurudi salama salimini. Anaongeza, kwa maombezi ya mama Maria msaada wa wakristo ndugu
hawa wanaweza kupata msaada na kurudi.
Pamoja na haya mashabulizi ya magaidi , Rais wa nchi Duterte amehairisha ziara yake
ya kwenda Moscow Urusi ili kuwa karibu na watu wake wa ufilippini kukabiliana na
kipeo hicho. Kikundi hicho cha magaidi kimesambaratika hadi kuchoma moto magereza
ya wafungwa na mashule mawili ambapo sasa wanajeshi wamezingira mji wote. Mkuu wa
Mkoa wa Marawi India amewaomba wanajeshi wasitumie mabomu katika mji huo wanamoishi
watu karibia raia 2000 zaidi wakiwa ni waislam.
Na nchini India hata matukio mengine kama hayo yametukia katika jimbo
Kuu la Hyderabad nchini humo na kaharibu Kanisa la Mtakatifu Mama Maria wa Fatima.
Ilikuwa ni siku ya Jumapili asubuhi 21 Mei 2017 kikundi cha watu kwa hasira karibia
100 waliingilia Kanisa lenye kupewa heshima ya Mama Maria wa Fatima katika Kijiji
cha Jimbo la Hyderabad. Washambuliaji hao waliharibu msalaba na kuvunja Sanamu ya
Mama Maria wa Fatima. Kanisa hili lilikuwa jipya ambalo lilitabarukiwa tarehe 13 Mei
2017 mwaka huu kwa namna hiyo ni uchugu wa jumuiya nzima na Askofu Mkuu wa Hyderabad.
Kanisa hili lilitabarukiwa tarehe 13 Mei 2017 na Askofu Mkuu Thumma Bala, siku ambayo
mama Kanisa Katoliki lilikuwa linaadhimisha miaka 100 tangu kutokea kwake mama Maria
wa Fatima.
Askofu anasema tendo la kuharibu sanamu ya mama Maria ni unajisi na inatia uchungu
na huzuni kwa hisia za waamini wote wa jumuiya. Aidha Askofu Mkuu anasema, baada
ya upelelezi wa maafisa polisi, watafanya liturujia ya kusafisha. Masikitiko makubwa
pia yamenoshwa na Sajan K. George Rais wa Baraza la Makanisa ya Kikristo nchini
India (Global Council of Indian Christians).
Kwa mujibu wa polisi, shambulio hili inaweza kutokana na mgogoro wa ardhi iliyojengwa
Kanisa jipya na kusababishwa wazalendo wenye itikadi kali kutopendelea ishara ya Kanisa
hilo. Lakini pia hizi ni ishara za kuonesha jinsi gani Wakristo wanaendelea kuonewa
pia kuwa na uvumulivu mkubwa katika nchi ya India.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |