2017-05-24 15:10:00

Mahubiri ya 24 Mei 2017, Sikukuu ya Mama Maria Msaada wa Wakristo!


Tarehe 24 Mei 2017 Kanisa Katoliki linafanya kumbukumbu ya sikukuu ya Bikira Maria Msaada wa Wakristo. Katika Basilika ya Mtakatifu Maria Msaada wa Wakristo huko Torino nchini Italia imeadhimishwa sikukuu hiyo kwa Ibada maalumu ya misa  ikiongozwa na  Askofu Mkuu Cesare Nosiglia wa Jimbo Kuu la Torino. Ni Mtakatifu Yohane Bosco wa Torino na mwanzilishi wa Shirika la wasalesiani aliye anzisha ujenzi wa mahali hapo patakatifu na kupewa jina la Maria Msaada wa Wakristo na ndivyo walipendelea kumwita mama wa Yesu.

Katika mahubiri ya Askofu Mkuu wa Torino anasema, kila mwaka sikukuu hii inatukutanisha pamoja chini ya miguu ya Maria Msaada wa Wakristo kama Kanisa la Torino kwa maana ya jumuiya ya wakristo, lakini pia hata kwa jamii yote ya mji kufanya sikuu ya kukumbukwa.
Injili iliyosomwa imekumbusha jinsi gani Mama Maria anato maombi kwa mwanae Yesu, kuwaombea vijana katika sikukuu ya ndoa ili kutatua matatizo yao ambayo hayakuwa ni madogo. Tangu mwanzo wa historia watu wamekuwa na ibada kuu ya kumheshimu Mama wa Mungu, wamempokea katika maisha yote ya kihistoria na daima wamekua katika mapokea hayo ya kuonesha umaa wa kweli. Watu wamemwona mama Maria kama kitulizo na matumaini ya maisha yao endelevu na yeye daima amekuwa msaada mkubwa hasa wakati wa matatizo na mahangaiko ya watu wengi. Kwa njia hiyo, Askofu Mkuu anawaalika waamini wote Kanisani kumkabidhi jimbo lote, mjini wa Torino na wote wanafanya ibada ya mama Maia Msaada wa wakrist ili kwa maombezi yake ya nguvu  waweze kupata ulinzi wake kwa kila tatizo la kimwili na kiroho, aidha yeye kuwa nguzo ya imani yao katika Kristo.

Anamkabidhi  Mama Maria Mkutano wa Vijana Kijimbo unaotarajiwa kufanyika, ambapo amewaalika vijana wote kuwajibika na kuwa wapya kiroho, kibinadamu na kijamii katika Kanisa na Ulimwengu. Uwajibikaji huo kwanza uanze na ujasiri wa kuhushudia imani yao katika yao na wengine, kwakufanya maamuzi ya  busara katika ngazi ya wito ambayo Bwana anawaita,ili wajikite zaidi katika shughuli za kuwasaidia wengine wanapokuwa na nafsi katika nyanja ya elimu, upendo na shughuli za kimisionari.

Amemkabidhi  mama Maria safari ya kichungaji ya Jimbo, inayojikita zaidi katika umoja na  makutano , ili waweze kukuza kila jumuiya kuwa na mahusiano mema kwa watu wote wahusika wa Kanisa, ambao ametaja kuwa ni mapadre, mashemasi, watawa , walei na kila aina ya vyama na mashirika yaliyomo ndani ya jimbo Kuu la Torino. Umoja ni zawadi kutoka kwa Mungu anasema, lakini unahitaji  mwendelezo wa juhudi kwa  kila mbatizwa ili kuweza kujenga kwa pamoja jamii iliyo bora na Kanisa imara. Kwa upande wa shughuli za kujikita ndani ya familia:ni lazima kutoa ushuhuda wa umoja katika upendo na imani katika jumuiya zote za kiparokia. Hiyo ni kwasababu Parokia ndiyo inafikiriwa kuwa familia ndani ya familia nyingi, na kila mkristo lazima kushiriki katika shughuli hiyo hai akiwa anatambua huduma halisi na wajibu wake kama mkristo aliye hai. Katika umoja wa kichungaji ni lazima kujita katika kuhamasisha zaidi ya yote haki na amani pia kwa ajili ya wengine ambao wamebaguliwa au kuathirika katika hali ya maisha yasiyo kuwa na matumaini endelevu.

Askofu Mkuu wa Torino amemkabidhi mama Maria wagonjwa, wanaoteseka ambao daima wako rohoni mwake Mama. Amekumbusha juu ya miaka 100 ya kutokea kwa Mama Maria wa Fatima. Anasema Mama Maria daima ametoa wito wa uongofu na kutubu ili kupata msamaha wa ulimwengu ambao hadi sasa bado kuna haja ya neema kwa idadi kubwa wa mahujaji wanaotoka pande zote za dunia kufika kila aina ya madhabahu ya Mama Maria. Kwa namna hiyo matukio hayo yanazidi kukumbusha wazi kwamba lazima kuwatazama watu na ndugu zetu wanaoteseka katika nyumba zao,mahospitalini au katika vituo vya wazee. Kuna haja ya kutoa upendo makaribisho na kuwa karibu kama zawadi na neema ya Kanisa na jamii nzima.

Aidha Askofu Mkuu amesema kwamba wamkabidhi Mama Maria watu wote wanaojikita zaidi katika kukabiliana na matatizo ya kijamii, kama vile kuulinda mji na  maeneo yote ambapo wakati mwingine siyo rahisi kwasababu kuna migongano na mgawanyiko. Aidha anaonesha wasiwasi  juu ya nyakati zijazo na kusema kuwa kunahitajika mshikamano, kukaribisha na  kuhamasisha amani.  Wazalendo wakristo kuanzia walei, kama wito wenyewe wa Injili wanaitwa kuongoza na kuelekeza au kukabiliana na  hali halisiya wakati kwa kujitoa na kutoa ushuhuda wa Kristo mahali walipo. Kwa njia hiyo anawaalika wasiwe tofauti katika kuwajibika, wawe kwanza mashuhuda wa Kristo ambapo wafungue njia zaidi za  upendo na mshikamano ambao ndiyo mihimili mikuu ya Injili.

Aidha anamkabidhi Mama Maria  watu wote pia waojikita katika kutunza na kupokea uhai  kwa heshima kuanzia kutungwa kwa mimba hadi mwisho wa maisha, bila kubagua mtu yoyote awe kabila, rangi , lugha na utaifa, utamaduni au dini.Halikadhalika amemkabidhi Mama Maria wale wote wanaojikita kulinda usalama wa mji na maneo yote katika kuelemisha juu ya sheria na hali halisi inayotakiwa katika maamuzi ya maisha ya kijamii yaliyo mema na utulivu kwa watu wote. Amemkabidhi Mama Maria Msaada wa Wakristo mashahidi wengi wa nyakati hizi ambao wanamwaga damu kwa ajili ya imani katika Kristo, anasema: sadaka yao iwe chachu ya maisha na amani kwa wote  na Injili ya huruma, msamaha na uongovu wa kweli  uweze kuwafikia wale wahalifu wanao fanya matendo ya kuua bila kujali au kusababisha vifo kwa watu wasio na hatia, ili neema ya upole na ukarimu kwa njia ya Roho Mtakatifu iweze kuwafikia.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.