2017-05-21 10:15:00

Wasiwasi wa Papa kuhusu mapinduzi ya kiteknolojia na dhana mpya kijamii


Tusiwe watazamaji tu bali kuwa mstari wa mbele  kutoa majibu ya dhati ili uchumi na masoko ya enzi  yenye kuwa na mapinduzi ya kweli katika ulimwengu huu yaweze kuwa daima katika huduma ya adhi ya binadamu. Ni wito wa Baba Mtakatifu Francisko wakati wa hotuba yake tarehe 20 Mei 2017 kwa wawakilishi 300 wanaoudhuria mkutano mjini Roma kutoka nchi 18 duniani katika kujibu maombi ya Baba Mtakatifu Francisko  kuhusu  Chama cha Mfuko wa Centesimus Annusi, wenye lengo  kukazia mafundisho jamii  ya Kanisa. Huu ni Mkutano wa 3 wa Mwaka wa Chama cha Centesimus Annus kwa ajili ya Papa , kilichoanzishwa kwa matashi ya Baba Mtakatifu Francisko miaka miatatu iliyopita.

Mara baada ya kuwakaribisha wote katika fursa hii ya Mkutano wa Kimataifa wa Centesimus Annus kwa ajili ya utume wa Baba Mtakatifu; anamshukuru Rais wa chama hicho Bw. Domingo Sugranyes Bickel kwa maneno ya hotuba yake aliyotoa: anasema anathamini juhudi yake ya kujaribu kutafuta njia mbadala ya uelewa kiuchumi, maendeleo na biashara ya masoko  ili kuweza kukabiliana na changamoto za kimaadili zinazotokana na kuibuka kwa dhana mpya ya nguvu inayotokana na teknolojia, na utamaduni wa matumizi mabaya ya maisha ambayo pia hupuuza maskini na kudharau wadhaifu (cfr Enc. Laudato si’, 16).

Watu wengi wanajibidisha kuunginisha familia ya kibinadamu katika umoja na kutafuta maendeleo endelevu ya kushirikisha kwa maana ya kutambua kwamba mambo yanaweza kubadilisha. Chama hicho kinatoa fursa yenye thamani na machango wa dhati ambao ufikiria , katika shughuli za masoko na uwekezaji , kwa njia ya mwanga na utajiri wa tamaduni wa  mafundisho jamii ya Kanisa na kwa ajili ya kutafuta namna nyingine yenye kujenga. Kulingana na ujuzi na uzoefu pia kwa kushirikiana na watu wengine wenye mapenzi mema, Baba Mtakatifu Francisko anaongeza; mmeweza kujikita katika kuendeleza mifano ya ukuaji wa uchumi unaozingatia utu, uhuru na ubunifu, ambao ndiyo wenye sifa ya utu na binadamu.

Taarifa yenu ya mwaka huu ambayo kwa hakika inajikita  juu  ya mapambano dhidi ya umaskini, kwa dhati inahitaji uelewa mzuri wa  matukio haya ya binadamu na siyo tu ya kiuchumi. Aidha Kukuza maendeleo muhimu ya binadamu inahitaji mazungumzo na kushirikisha mahitaji na matarajio ya watu. inahitaji kusikiliza maskini na matatizo yao ya kila siku ambayo ni uzoefu mbalimbali wa kukosa mahaitaji ili   kupanga majibu mahsusi kwa ajili ya hali halisi. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko anasema hii inahitaji kujenga maisha,kati ya jamii na ulimwengu wa biashara, miundo mbinu ya kuleta upatanisho wenye uwezo wa  kuweka pamoja rasilimali  na watu, kuanzisha mchakato ambao maskini ni wahusika wakuu  ndiyo walengwa. Kama mbinu ya shughuli za kiuchumi, zinalenga mtu na kumtia  moyo katika  mpango na ubunifu,ujasiriamali na jamii ya kazi na biashara hivyo ni kukuza ushirikishwaji wa jamii na ukuaji wa utamaduni wa mshikamano ufanisi.

Katika mkutano wenu mmezingatia maswala muhimu ya ajira katika mazingira kwa  mantiki mpya ya  mapinduzi ya kiteknolojia inayoendelea. Hatuwezi kutokuwa na wasiwasi juu ya tatizo kubwa hili la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana na watu wazima ambao pia hawana zana na rasilimali za kujiendeleza wao wenyewe. Ni tatizo ambalo kweli limekumba kiasi kikubwa cha watu wote ikiwa pamoja na nchi zilizoendelea na zile ambazo zinaendelea. Inahitaji kuendelea kujiuliza namna ya kukabiliana kwa maana ya kutafuta haki kati ya vizazi na wajibu wa siku zijazo
Vilevile sambamba na hiyo jitihada za kukabiliana kwa pamoja masuala yanayo husiana na ukuaji wa teknolijia mpya, mabadiliko ya masoko na matarajio ya wafanyakazi  inapaswa kuzingatiwa , na siyo kwa mtu mmoja bali ni kuzingatia familia kwa ujumla. Baba Mtakatifu amekumbusha kwamba wasiwasiwasi huu, pia ulijionesha katika Sinodi ya Maaskofu kuhusu familia , ambayo ilionesha wazi mazingira ya kutokuwa na kazi yanaleta shinikizo na matatizo ya familia na  athari za ukosefu wa ajira. 

Baba Mtakatifu Francisko amemalizia hotuba yake akiwatia moyo wapeleke  juhudi zao kwa njia ya mwanga wa Injili na utajiri wa mafundisho  jamii  ya Kanisa  katika masuala haya mazito na kuchangia mijadala, utafiti na mazungumzo lakini pia katika juhudi ya  kushiriki katika mabadiliko ya tabia ,maoni na namna ya kuishi  maisha ambayo ni muhimu katika kujenga dunia ya haki, uhuru na amani.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.