2017-05-21 10:27:00

Centesimus Annus: Ajira na uadilifu wa binadamu katika nafasi ya digital


Katibu Mkuu wa Vatican Pietro Parolini katika Mkutano wa tatu  wa Kimataifa wa uchumi na jamii ulioandaliwa na Chama cha Mfuko wa Centesimus Annus,kwa ajili ya Baba Mtakatifu  tarehe 18 Mei 2017. Ametoa hotuba yake akianza na shukurani kwa kukaribishwa kuhutubia katika tamasha la kuwakabidhi zawadi ya Kimataifa washindi watatu kwenye Mkutano wa  uchumi na Jamii ambao sasa ni miaka  mitatu  katika nafasi ya Mkutano wa Mwaka wa chama. Kardinali amesema; Mkutano wa mwaka huu umeongozwa na kauli mbiu “Njia mbadala ya ujenzi katika zama za mtikiso. Ajira na uadilifu wa binadamu katika nafasi ya digital na motisha kwa mshikamano na wema wa kiraia”.

Amefurahia kuona katika ukumbi huo washindi watatu Profesa. Markus Vogt, Padre Dominique Greiner na Dak. Burkhard Schäfers. Na kusema kwamba kila mmoja wao katika nafasi ya utafiti au kazi na katika maendeleo ya taaluma yake , wamesaidia kutoa majibu ya maswali yenye kuleta wasiwasi unaotokana  na maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia katika muhongo wa XXI, katika enzi hizi baadhi watu wengi wameonesha kuwa ni kama  ile ya mapinduzi ya nne ya viwanda.    Mbele ya tabia  zilizopo kwa sasa za kutafsiri, sura halisi za kijamii kutokana na dhana ya kiitikadi, kuwa uwiano mpana kati ya wa mwanafalsafa Max na uhuru huria , katika ziku za nyuma na leo ambapo tunaweza kuita ni teknolatria inayotafuta kuunda itikadi mpya, kama sayansai. Washindi wamechangia kuimarisha njia ya kufikiria tabia yenyewe ya mafudisho jamii ya Kikristo, ambayo inajibidisha kutatua matatizo ya kijamii kwa kuzingatia vipimo tofauti na kuoanisha heshima na hadhi ya binadamu.

Pamoja na majadiliano  na  kushirikishana wakati huu wa Mkutano wa Chama cha Mfuko wa Centesimus Annus , Kardirnali Parolini anaongeza kwamba mkutano huo unamfanya akumbuke Azimio la 2017 la kujenga njia mbadala ili kukuza hadhi ya binadamu, ambayo inatoa nafasi kubwa kwa ajili yake. Hiyo siyo ya itikadi na mbinu za kisayansi jamii tu au kama vile mazoea ya kisiasa na kiuchumi bali ni njia ya  kuweza kwa dhati  kufanya matendo mazuri kwa ajili ya wema wa wote. Kardinali Parolini, anatoa shukrani kwake Baba Mtakatifu Franciko kutokana na mafundisho yake na  ushauri  ambao umetoa majibu na kuonesha uhai wa fikra za ujasiliamali kikristo. 

Kwa hakika hii ni njia inyotaka kushirikisha wote watendaji kijamii na hasa wajasiriamali, siyo kwa dhamira ya kuongeza juhudi za kutoa huisani bali ni katika kukabiliana kwa  namna ya usawa wa mapato, pamoja na kutambua Azimo hilo linaoongoza katika mazingira magumu ya watu wengi na familia, hata katika nchi zilizoendelea. Kardinali Parolini anaongeza; ni lazima kuwanza kuwa na roho ya ukarimu: na katika Injili inatupa mfano wa Zakayo ambaye kwa mtazamo wa Yesu , alipata hisa ya kushirikisha nusu ya utajiri wake na masikini. Kwa njia hiyo kuna umuhimu wa kuwatia moyo wahisani na watu wanaojitolea , ambao mara kwa mara katika matokeo ya mazungumzo ya kina wapo katika Chama cha Mfuko wa Centesimus Annus.

Kwa hali hiyo, anatoa pongezi kwa niaba ya Baba Mtakatifu kwa mchango upatikanaji  mwaka 2016, na kwamba Chama hicho kimetoa mchango wake kwenye matendo ya huruma ya Papa hasa kwa ajili ya masaada wa wakimbizi zaidi kwa watoto wasio kuwa na msindikizaji .Aidha naye pia anaunganika naye kuwatia moyo chama hicho kwa shughuli nzuri iliyoanzishwa na Baba Mtakatifu Francisko.
Zaidi ya hayo anasema Kardinali kwamba,  Baba Mtakatifu kama aombavyo, inahitaji hatua za haraka ili kusaidia maskini na kuwa watendaji wa kwanza kwa hatima yao. Juu ya mipango ya sayansi  kijamii, inahitajika kutambua mbinu mpya za kuwahudumia na pia  uchambuzi na kipimo, ambavyo vinahusiana na uzoefu wa hali alisi ya wadhaifu.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.