2017-05-19 17:29:00

Kard.Filoni: Pongezi kwa Kanisa changa lakini lenye imani kubwa


Kardinali Fernando Filoni, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu, ambaye yuko katika hija ya kitume nchini Equatorial Guinea kuanzia tarehe 18 hadi 25 Mei 2017, amekutana huko Malabo na Mapadre na watawa  na kutoa hotuba yake Ijumaa 19 Mei 2017 akiwasalimia  wote wakiwemo maaskofu na kwa namna ya pekee Balozi wa Vatican katika nchi humo Askofu mkuu Juan NSUE EDJANG MAYÉ na kuwapa salam kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko.  Na kwamba anayo furaha kuwapo katika nchi hiyo ambayo Kanisa lake ni changa ikiwa ni kwa mara yake ya pili kuitembelea. Aidha furaha yake kubwa ni  kuona kuwa  Jumamosi  20 Mei 2017  ataadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa kuwaweke wakfu maaskofu wapya watatu walioteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko hivi karibuni!

Anasema amechagua kuanza na mkutano nao ili kuweza kuingia moja kwa moja katika Kanisa mahalia kwa njia ya wachungaji wake maana wao ndiyo msingi wa mazungumzo naye , kuwasikiliza , na kushirikishana furaha , wasiwasi na matumaini yao. Kwa kufanya hivyo ni pamojana na kuonesha mwito wa Baba Mtakatifu alio nao kwa Kanisa lote mahalia kama Kanisa na Familia ya nchi ya Equatorial Guinea. Kanisa lenu katika taifa hili kwa upande mwingine inatia moyo kutokana na kuendelea kuongezeka kwa imani pamoja na mabadiliko muhimu wa Injili na katika utume. Matokeo ya shuhughuli hizi ni kutokana na mchango wa kazi yenu Mapadre, na watawa mnayoendelea kufaya kwa kijibidisha kwa kina.
Anawashukuru kwa mchango wao wenye thamani kubwa ya  kutoa maisha na katika utume wa Kanisa.

Anawashukuru kwa mchango wao wenye thamani kubwa  hasa ya  kutoa maisha yao na katika utume wa Kanisa.Lakini pamoja na hayo ytoe, Kardinali Filoni anasema ;anataka kuyataja baadhi ya matatizo yaliyojitokeza wakati wa mchakato wa kuwachagua maaskofu wapya yaliyotolewa kutoka kwao kumpelekea Balozi wa kitume.Waliandika kwamba, wapo makuhani ambao wanaishi maisha mabaya ya kiroho, kuna utengano, wivu, chuki , kupendelea sifa na madaraka kwa baadhi ya makuhani na watu walio wekwa wakfu. Hayo yote Anaongea kusema Kardinali taratibu yamesababisha kuanguka kwa maadili mema kwa upande wa mapadre na watawa,kwa maana nyingine wamegeuka kuishi kama watu wa kiulimwengu na maisha ya kujiendeleza binafsi badala ya  maisha ya kitume.

Kwa njia hiyo Kardinali  Filoni anatoa ushauri wa kutia moyo, kama ushara ya kuwa karibu nao ya kibaba. Anasema, kama makuhani, watawa na wahusikia wa Kanisa mahalia wanaitwa kuwa chumvi na mwanga ( Mt 5,13-15) katika jamii hiyo kwa kufuata mfano wa Yesu mchungaji mwema (Yh 10).Ni lazima kuishi kwa uaminifu,furaha na utambulisho wa kikuhani na kiutauwa. Aidha anaongeza; Kanisa kwa asili yake ni ya kimisionari, kwa njia ya ujilishaji na ndiyo inapaswa kupewa  kipaumbele. Baba Mtakafiu Francisko katika Waraka wake wa Furaha ya Injili ameeleza vizuri ambapo Kanisa la Malabo na kwa nchi yote ya Equatorial Guinea inaalikwa  kutembea katika njia ya uongofu  kwa kujibidisha kwa nguvu katika uijilishaji. Ni lazima kumtangaza Kristo hadi ya pembezoni. Pamoja na kutafakari imani ya wakristo, wazalendoa wenu wanayo kiu ya kuona, kukutana na kuamini Yesu. Je wanawezaje kuamini bila kusikia wanasema? , wanawezaje kusema bila kusikia anayetangaza? (Rm 10,14-15). Kama anavyokumbusha Baba Mtakatifu Francisko, siyo kulazimisha imani yao bali kwa kutangaza neno na kutoa ushuhuda, kwasababu Kanisa halikui kwa njia ya propganda. Kanisa linakua kwa njia ya ushuhuda wa kila mmoja anao utoa kwa watu wa Mungu.

Aidha kati ya maneno mengi ya shuhuda wenu, Kardinali amesema, ni vema kubainisha katika maisha ya kiroho, kimaadili na kichungaji. Kardinali Filoni amesema;ni lazima kuishi katika Roho na kutembea katika Roho kama anavyofundisha Mtakatifu Paulo (Wagalatia 5,25). Kwa maneno hayo Mtakatifu Paulo anatakumbusha kuwamba maisha ya kiroho ya kuhani au aliyetiwa wakfu lazima yaongozwe na Roho wa Mungu ambaye anampeleka katika utakatifu, zaidi ya kuwa mwaminifu, wanaitwa katika utakatifu na  ndiyo utambulisho kwasababu wamepakwa mafuta ya matakatifu na pia  kutumwa kutangaza Injili. Ninyi mmeitwa kushi na kuajibika katika kutangaza injili, kwa kufuata mfano wa Kristo masikini msafi na Mtiifu. Kuhani zaidi ya yote anaitwa kuwa na kama Kristo ambaye ni  kuhani Mkuu hata milele. Kama ni kuhani lazima kuwa na uhusiano wa kina na Yesu mchungaji Mkuu, na  Mkuu wa Kanisa , kwa maana nyingine ni kuishi kama moyo wa Kristo; kupenda kama anavyopenda, kufikiria na kutenda kama Yesu atendavyo na afikiriavyo, kuhudumia kama Yesu anavyohudumu kila wakati katika maisha.

Kama asemavyo Baba Mtakatifu Francisko ya kwamba moyo wa mchungaji Kristo anatambua njia mbili tu nazo ni Bwana na watu, kwa maana hiyo moyo wa Kristo uwekwa muhuri wa upendo wa Bwana katika nafsi zenu, ambao haujipendelei wenyewe bali ni kutazama Mungu na ndugu (Mahubiri Papa Francisko :Jubilei ya mapadre 3Juni 2016). Kardinali Filomi anafadanua zaidi; ukuhani siyo kazi au shughuli za kufanya kwa wakati tu na kuishia hapo. Ukuhani ni mtindo wa maisha na siyo kazi. Ili kuishi kwa kina utambulisho huo wa kikuhani maisha ya kiroho ya kuhani lazima yashikamane na sala, kusikiliza Neno la Mungu,kwa mfano wa Mama Maria alivyosikiliza.

Kuhusiana na maisha ya kiroho , Kardinali Filoni amelezea juu ya useja. Uchaguzi huu unapaswa kufikiriwa kwa mantiki ya mahusiano ya usafi uliopo katika daraja Takatifu ambalo litnatoa utambulisho wa kikuhani wa Yesu Kristo mkuu na mchumba wa Kanisa. Kanisa kama Mchumba wa Kristo, linahitaji kupendwa na kuhani kwa namna ya kipekee kama alivyo Yesu Mkuu na mchumba alivopenda. Kwa maana hiyo Mapadre na watawa wanapokea useja kwa utashi  wao na uchanguzi wao wa upendo kila wakati. Wakiwa wanatambua udhaifu  wao na hali ya kibinadamu. Lakini tunatambua kwamba ili kuishi mahitaji ya kimaadili ya roho kichungaji katika useja wa kikuhani, ni lazima  sana kuwa mtu wa  sala ya kinyenyekevu na kuamini. Ili kuweza  kuimarisha ukuhani, ni lziama kujikita katika mahusiano ya kindugu, ndugu padre na katika maisha ya utauwa. Ndugu kaka na dada wa kuishi pamoja katika jumuiya ndiyo neema ya kutemba katika maisha yenye thamanaini ya fumbo hili.

Halikadhalika anabainisha kwamba, mahali ambapo panakosekana uhusiano mwema kati ya makuhani na watawa ddipo uanza kipeo cha matatizo. Kwa njia hiyo inabidi kutunza mahusiano mazuri na Maaskofu wao, wakuu wa mashirika kwa uaminifu kama Baba Mkuu wa  Kanisa mahalia.
Pia anabainsha hatari za kupoteza furaha wakati wa  utume wenyewe, na kwamba utafikiri kazi ya kuinjilisha ni kama sumu mbaya balada ya kuwa ya furaha ya kuitikia upendo wa Mungu anayetuma kwenda katika utume wake ili kuzaa matunda mema.Anaeleza bayana kuwa wengine kweli wamepoteza uzoefu huo na mwisho wao wameona utume kuwa mchungu. Ili kuweza kujikita katika maisha yote kwa nguvu katika huduma ya Kanisa ni lazima kuwa na upendo wa kichungaji wa Yesu aliyetoa maisha kwa ajili ya zizi lake. Ni lazima kuiga Yesu kwa ujitoa bila kubakiza katika huduma yake. Ni kwa njia ya huduma ya kichungajji itakayo leta utajiri wa  utume na huduma ambayo inatendeka, kwa namna ya kufikiri, kushirikiana na watu wengine ambao mmeitwa kuwatumikia.

Kardinali Filoni anasema; kwa njia hiyo upendo unahitaji uongofu wa kitume; inabidi kutoka nje na kwenda kukabiliana na hali halisi kwa ujasiri ili kuwafikia wengi walio pembezono ,wanaohitaji msaada wa mwanga wa Injili. Jambo kubwa na msingi wa upendo wa kichungaji unajikita hawali ya yote katika masikini, walio baguliwa, wadogo,wagonjwa, wenye dhambi na wasio kuwa na imani. Upendo wa kichungaji unafanya sisi tuwe  zaidi tayari kubeba aina ya huduma yoyote kwa manaufaa ya Kanisa na roho za watu. Ni lazima kuwa makini na hasa katika matukio yanaoyozidi kutokea kwenye harakati za kuzuka kwa madhebu mengine. Kardinali anauliza swali, Je hayo yanatotokea  kutokana na kwamba mapadre na watwa wamekwenda mapumziko? Hivyo ni wito kwa maaskofu wote kutafakari kwa makini ili asiwepo hata mmoja aliyekimbia Kanisa la Baba na aweza kupotea daima.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.