2017-05-18 16:14:00

Papa: Wagonjwa mnayo thamani kubwa machoni pa Mungu!


Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na wagonjwa wa "Huntington" na familia zao kutoka nc tarehe 18 Mei 2017. Katika Hotuba yake, anawashukuru wote walio wezesha kuandaa mkutano huo na takafakari inayohusu wagonjwa wa Huntington. Aidha ametoa shukrani kwa Bi Cattaneo na Bw.Sabine kwa maneno ya hotuba ya utangulizi wa mkutano huo. Amewasalim watu wote ambao katika miili yao wanabeba ishara ya magonjwa, pia wengine wenye mateso ya magonjwa nadra. Anatambua kwamba wengi wao wamekabiliana na safari ndefu na ngumu isiyo rahisi ili waweze kuwapo katika mkutano huo na yeye. Amewashukuru sana kwa uwepo wao. Baba Mtakatifu aidha amesema kuwa, amesikiliza kwa makini historia yao na mateo yao ya kila siku wanayokabiliana nayo na kutambua jinsi gani familia zao wanajitahidi kuwa karibu  nao, pia madaktari , wahudumu wa afya na watu wa kujitolea ambao wako karibu nao katika safai yao yenye milima ya kupanda na migumu.

Kwa bahati mbaya woga na matatizo ambayo yamesasbabishwa maisha ya watu walio na ugonjwa wa Huntington , yameunda tabia ya kutoelewaka, vizingiti, na hata ubaguzi wa kweli. Kesi nyingine za wagonjwa na familia zao wameishi kipeo cha aibu , upweke na kutelekezwa. Baba Mtakatifu Francisko anasema lakini ,leo hii wako pale  kusema kuwa tunataka kutoa sauti  kwa dunia nzima kwamba  hakuna tena kujificha, na hii siyo kwamba ni kauli mbiu rahisi tu, bali ni wajibu ambao lazima hufanyike na wahusika.  Uhakika na nguvu ya kutamka maneno haya yanatokana na usahihi wa maneno ya Yesu aliyotufundisha yeye mwenyewe. Wakati wa utume wake alikutana na wagonjwa wengi, alichukua jukumu la kubeba mateso yao, alivunja ukuta wa kunyanyapaa na kubaguliwa ulio kuwa unazuia wengi wajisisikie kuheshimiwa na kupendwa. Kwa upande wa Yesu wagonjwa hayakuwa vikwazo vya kukutana na mtu bali ilikuwa ni kinyume chake. Yeye alifundisha kwamba maisha ya binadamu daima ni yenye thamani, mara zote inahitaji kupewa adhi na hakuna mtu au kitu chaweza kuondoa adhi hiyo na hata ugonjwa. Udhaifu siyo kitu kibaya Baba Mtakatifu Francisko anaeleza. Magonjwa au udhaifu ujieleza ambapo ni lazima kutosahau kwamba Binadamu anathamani kubwa  machoni pa  Mungu isiyo na kifani.

Hata wagonjwa inawezakana ikawa fursa ya kukutana, kushirikishana na kuwa na mshikamano. Wagonjwa waliokuwa wanakutana na Yesu walikuwawapya na zaidi walikuwa na utambuzi. Walikuwa wakijisikia kusikilizwa, kuheshimiwa na kupendwa. Hivyo Baba Mtaktifu Francisko anawaambaia kwamba; kamwe mmoja wenu ajisikie  kuwa peke yake, kuwa mzigo wa mwingine na kutamani kutoroka Kwasababu  ninyi ni wenye thamani machoni pa Mungu na thamani machoni pa kanisa. Akiwageukia wanafamilia wanaoishi na ndugu wagonjwa wa Huntington anasema Baba Mtakatifu kuwa, jueni kwamba hakuna mtu anayeweza kweli kushinda upweke na kukata tamaa kama hana mtu au timu ya watu wenye kujituma na kuwa na uvumilivu katika kuwasikiza kwenye safari yao. Ninyi nyote ni baba , mama mke mme, watoto na  ndugu ambao kila siku kwa ukimya mnajikita kwa dhati lakini kwa ufanisi mnawaongoza katika safari hiyo ngumu kuwasindikiza wanafamila wenu. Hata nyinyi wakati mwingine safari hiyo ni mpando, na kwa maana hiyo ninawatia moyo ya kwamba msijisike peke yenu, na msingie  katika vishawishi vya ya hali kuona aibu au hatia. Familia ni nafasi ya upendeleo wa maisha na heshima, na mnaweza kufanya kazi pamoja ili kujenga mtandao wa mshikamano na msaada  ambao ni familia peke yake yenye uwezo wa kuutoa kwa maana ndiyo ya kwanza kuitwa kuishi.

Baba Mtakatifu Francisko akiwageukia madaktari na wahudumu wa wafya na watu wa kujitolea wa vyama vinavyojihusisha na ugonjwa wa Huntington na walio athirika na ugonjwa huo amesema kati yao kuna hata wahudumu kutoka Hospitali ya wagonjwa ya Padre Pio ambayo inasaidia katika utafiti na pia kwa mchango wa Huduma hiyo kutoka  Vatican katika eneo hili muhimu sana. Amewaelza kuwa  huduma yenu nyote ni yenye thamani kwani kwa uhakika katika bidii yenu inachukua sura  kwa namna halisi na kuleta matumaini  kwa wanafamilia ambao wanawategemea, wanawaamnini na wamewakabidhi wagonjwa wao. Changamoto za uchunguzi na huduma za matibabu muhimu kwa wagonjwa lakini bado inahitajika nyingi.
Bwana awabariki kazi yenu, na pia mnaweza kuwa kiini kwa wagonjwa na familia zao ambao kwa hali tofauti wanakakabiliwa na majaribu ya magonjwa ambapo inahusisha hata mantiki ya kijamii na kiafya ambayo mara nyingi unakuta siyo kipimo cha adhi ya binadamu. Baba Mtaktifu kwa hili anaongeza akisema; hata hivyo katika magonjwa bado inaongeza matatizo ya umaskini, utenganishaji wa kulazimishwa na kuleta hali ya kutokuaminiana. Kwa hiyo vyama na mashirika ya kitaifa na kimataifa ni muhimu. Ninyi ni kama mikono ambayo Mungu natumia kuwapa matumaini wagonjwa. Ninyi ni sauti ya watu hawa ambao wanadai haki na zao.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.