Wito wa nguvu kwa nchi zote za Jumuiya ya kimataifa ili waweze kutoa kipaumbele
cha kupambana na unyanyasaji kijinsia na pia vurugu, ameutoa Askofu Mkuu Bernadito
Auza Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Baraza la Umoja wa Mataifa huko New York.
Askofu Mkuu ametoa hotuba hiyo mapema wiki hii katika Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa wakati wa majadiliano kuhusu mada ya “wanawake, amani na usalama”.
Askofu Mkuu anasema ,ni mateso makubwa na yasiyoelezeka kwa upande wa wanawake wanao
endelea kuathirika kwa ukatili wa kiajabu ambapo siyo rahisi kuweka moto huo chini
ya miguu na kufumba macho bila kuwa na msukumo wa kuinglia kati.
Kwa nguvu zote Askofu Mkuu Auza amehusisha juu ya ripoti ya mwisho iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kuhusu unyanyasaji wa kijinsia na katika vita. Amebainisha kuwa hali hii inahitaji utelekelezaji wa haraka kwasababu ameorodhesha matukio hayo kuwa ni pamoja na utekaji nyara, husafirishaji wa watu, utumwa wa ngono, ukahaba , utoaji wa mimba ,ugumba wa kulazimisha na ndoa za kulazimisha. Kwa mantiki hiyo Askofu Mkuu Auza anasema ni tishio na uhalifu mbaya usiolezeka kwa kuzingatia matumizi ya unyanyasaji wa kijinsia kama mbinu za ugaidi.Uhalifu huu hasa wa matendo yaliyotajwa katika ripoti ni kama litania ya maovu.
Hiyo ni kwasababu inaonesha ni jinsi gani kuna haja ya kuhamasisha dhidi ya za magaidi ambao wanazdi kutishia kugawanya watu, kulazimishwa watu kubadili dini au mabadiliko kwa njia ya ndoa ,kukandamiza haki msingi za wanawake, magaidi kupata faida kwa njia ya biashara ya ngono ,magaidi kuwanyang’anya watoto ndani ya familia na kuwafanya wanyamaze , au kutoa wasichana wawe wathirika katika kupigana kwenye vita kwa fidia, magaidi kuwatumia wanawake au wasichana kama wanavyotaka pia kuwatumia wasichana kama ngao za binadamu kwa manufaa yao kwenye mabomu ya kujitoa muhanga.
Kwa njia hiyo Askofu Mkuu anasema kuna ushahidi mwingi wa kuthibitisha kwamba
wanawake na wasichana ndiyo walengwa kama mbinu ya kujenga hofu ambayo huleta uharibifu
kwa utashi wao na kuwafanya kama mashine za magaidi wanaopata kipato kwasababu ya
kuwatumia.
Katika kukabiliana na majanga haya kwa utambuzi huu wa vurugu na mateso Askofu Mkuu
mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Baraza la Umoja wa Mataifa New York anamalizia
akiwa na matumaini kwamba katika ulimwengu wa wanawawake na wasichana ambao adhi
yao imekiukwa, Baraza la Usalama wanaweza kuingilia kati na kwamba matumaini yake
yasiwe ya bure.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |