2017-05-13 15:22:00

Taasisi za Elimu ya Juu za Kikristo na Kiislam kuanzisha mtandao


Katika mji wa Amman, nchini Jordania, umezinduliwa  mtandao wa kudumu kati ya Taasisi na vituo vya mafunzo ya elimu ya juu katika vyo vikuu vya Kiislam na wahudumu wakristo wanaosoma au kufanya kazi katika nchi za Uarabuni. Hayo yamefanyika wakati wa Mkutano katika kituo cha Kimataifa cha mazungumzo cha  Kaiciid na Diyar Constortium hivi karibuni. Jukumu muhimu la Taasisi za Elimu ya Juu yenye asili ya dini katika maisha ya kila siku ni kupinga juu ya kuchakachua masuala ya kiteolojia na Mafundisho ambayo kwa muda mrefu viongozi wa kisiasa wamekuwa wakialikwa kuchambua na kutafuta mbinu na hatua ambazo wangeweza kujiuliza jinsi ya kuondokana na migogoro ya kidini ambayo ndiyo mama wa marumbano y amara kwa mara katika bchi hizo.

Onyo hilo  pia limetolewa hata kwa upande vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ambayo mara nyingi imekuwa ikikanusha ukweli huo na kutofuata wito, lakini ki ukweli ndiyo asili ya kufanya kampeni za kuchochea chuki za kidini ambazo uongeza vurugu na vita vya kidini.
Kwa njia ya kuweka mikakati ya ushirikiano, wa vituo vya  Diyar na Kaiciid wameunganisha wawakilishi kutoka katika taasisi za elimu ya juu ya kiislam na wakristo kwa ngazi ya vyuo vikuu vilivyoko katika chi za Kiarabu na nyingine ili kutafuta njia za pamoja katika Taasisi za Kidini zilizo wazi katika kutafuta umoja na  utamaduni na pia wepesi wa kuhamasisha  wema wa haki ya kila mzalendo.

Mtandao huo  unaunganisha wanachama wa Taasisi ya elimu ya juu ya Chuo Kikuu zenye kuwa na matawi yake katika nchi za uarabuni, lakini miongoni mwao kuna hata chuo cha Kiislam cha Sharia na mafunzo ya Kiislam(College of Sharia and Islamic Studies) Qatar; Chuo Kikuu cha Sheria nchini Jordania; Taasisi ya chuo Kikuu cha Kidomeincani cha masomo ya Mashariki kilichopo Mjini Cairo. Tawi la Chuo Kikuu cha  Masomo ya dini cha Notre Dame kilichopo Lebanon, Chuo Kikuu cha Ez-Zitouna (Tunisia, Chuo Kikuu cha Kiilsam Abdullah Bin Yassin (Mauritania) na Chuo Kikuu cha Kiinjili (Evangelical Theological Seminarry  Cairo).

Wawakilishi wa taasisi wameweka lengo la kazi ya miaka mitatu ya mikutano na vikao vya kazi  ili kupanua mpango kwa lengo la kuendeleza miongozo ilivyoainishwa katika siku ya mkutano huo. Ili kukabiliana na utata wa mtandao na kugundua vyombo vya habari na mitandao ya  kijamii katika nafasi ya majadiliano na maelewano kwenye utambulisho tofauti, Kaiciid  mwaka jana  walifanya mjini Amman mpango wa kwanza wa mafunzo kwa ajili ya wandesha sekta iitwayo Umoja dhidi ya vurugu kwa jina la dini.  Kozi hiyo ya utafiti ilikuwa na lengo kubwa la kusambaza misingi na mikakati imara katika tovuti  zenye kueneza na kuchochea chuki za kidini ili wapate  kutambua ubora na wingi wa utamaduni na dini za Mashariki ya kati kama utajiri wa maisha ya binadamu na mshikamano.

Kituo cha Kaiciid kilifunguliwa mwaka 2012 huko Vienna nchini Austria; ambacho pia kimeanzishwa Saudi Arabia, Hispania na Austria, kuna mwakilishi wa kudumu ambapo pia wawakilisha wa madhehebu makubwa ya  Wakristo, Budha, Wahindu, Wayahudi na Waislamu.
Diyar Consortium, ni shirika la kiekumene, kinachoendeshwa na Wakristo wa  Kilutheri kilichoanzishwa huko Bethlehemu  mwaka 1995. Kinajiuhusisha na kushiriki katika  programu za kusaidia makundi yaliyoathirika zaidi kutoka nchi ya Palestina.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.