2017-05-12 15:21:00

Padre Adolph Ntahondereye aliyekuwa ametekwa nyara amefariki dunia!


Padre Adolph Ntahondereye Paroko msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Francisko Saverio, Burundi Magharibi mpakani mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amefariki  terehe 11 Mei 2017 baada ya wiki mbili kuachiwa huru kutokana na masumbufu na mateso aliyopata akiwa mikononi mwa wateka nyara.
Kwa mujibu wa Askofu Mkuu  Ngoyagoye Evariste wa Jimbo Kuu la Bujumbura anasema, Padre Adolph hakuacha kitanda alichokuwa amelazwa tangu kuachwa huru, amekufa kufuatia mateso makubwa ya safari ndefu iliyo mwathiri kiroho na kimwili. Tarehe 9 Aprili 2017  Padre Ntahondereye alitekwa nyara pamoja na watu watatu mara baada ya kupata ajali  barabara iliyokuwa imetayarishwa katikati ya Barabara na kikundi cha watu wenye silaha wakiteka mabasi. Watu wengine watatu waliokolewa baada ya siku 17 wakiwa mateka.

Kwa mujibu wa mtekwa nyara Mathias Mijuriro anasema, Padre Adolph alitoka mateka akiwa tayari ameathirika sana kiroho na kimwili. Kwani wakati wa safari watesi wao walimlazimisha kutembea kwa miguu kilometa nyingi sana kwenye milima inayotazama mji wa Ubvira karibu na nchi ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kutokana na mkusanyiko wa uchofu mwingi, padre alipata shida sana kutembea hadi wateka nyara kumsaidia aweze kutembea . Anaongeza akisema; kama yeye asingekuwa ni mazoea ya kutembea kila wakati, angeishia katika hatari ya mauti iliyo mfikia Padre Adolph kwenye safari ndefu ya milima ya Gatumba- Bujumbura.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.