2017-05-11 10:09:00

Jukwaa la V la Dini Kimataifa kwa ajili ya utetezi wa watoto Panama!


Karibia viongozi 430 kutoka  madhehebu makubwa ya dini duniani na watoto 60 kutoka  nchi 70 , wakiwemo wawakilishi wa Kimataifa , wamemunganika katika Jukwaa la V la Mtandao wa Dini Kimataifa Mjini  Panama kijifunza hatua gani za kuchukua ili kuondokana na aina zozote za ukatili dhidi ya watoto.Hili ni Jukwaa la V la Kimataifa la madhehebu ya dini linalojikita katika utetezi wa watoto duniani katika masuala halisi yanayowakumba hasa ukosefu wa haki zao na mateso. Mkutano huo umefunguliwa na tarehe 9 Mei 2017 na Askofu Julio Murrey kutoka Baraza la Maaskofu wa Panama  na unamalizika tarehe 11 Mei 2017. Lengo la Jukwaa hili liloandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali ni kutaka kujenga dunia iliyo bora kwa kwa ajili ya watoto ambao ndiyo waathirika wa kwanza  na kutokomeza aina za ukatili na ghasi wanazotendewa.

Mada mbalimbali za kujadili zilizotumwa  kwakwe Rais wa Arigano Mh. Keish Miyamoto ni: ulinzi wa watoto dhidi ya  vikundi vyenye msimamo mkali, vurugu za makundi yenye silaha na uhalifu wa kupangwa, kukuza hali ya roho ya utu wem, kukomesha vurugu, unyonyaji na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto. Padre Katoliki Sidney Fones kutoka nchi ya Chile ambaye ni muhusika wa Kamati ya Maandalizi ya Jukwaa hilo anasema, lazima watu kuelewa kwamba wanayo nafasi muhimu ya kuhakikisha amani inapatikana kwa ajili ya watoto,na wapate haki msingi za maisha na pia kulindwa. Aongeza, ni matumaini ya kwamba baada ya Jukwaa hilo mawazo na matokeo yanaweza kuleta matendo ya dhati na hasa matunda yake  kwa ajili ya ulinzi watoto wote duniani ambao ni waathirika  wa kunyonywa, kutumikishwa watoto wadogo katika kazi ngumu, pia kufanyiwa matendo mengi ya kikatili na yasiyo ya kiutu.

Kabla ya Mkutano huo watoto 60 na vijana kutoka nchi 13 walishiriki katika maandalizi ya Jukwaa ambapo waliweze kuwaandaa  mkataba baina ya dini ili kuweza  kuwakilisha tarehe 11 Mei 2017 wakati wanamaliza Jukwaa. Mkataba huo wa pamoja ni kutaka kijikita katika uwajibikaji kwa kila mmoja katika ujenzi wa dunia iliyo bora, isiyo na vurugu wala ghasia dhidi ya watoto. Mkutano kama huo wa kidini kimataifa umefanyika katika baadhi ya nchi ya Tokyo Geneva, Hiroshima na Dar es Salaam Tanzania.

Jukwaa la Mtandao wa dini Kimataifa ulianzishwa mwaka 2000 wenye kuwa na washiriki wa dini kubwa duniani kama vile, wayahudi, waislam, wakristo na wabudha. Mtandao huo utengeneza mipango Kikanda pia katika maeneo ya pembezoni, hatma yake ni kuboresha maisha ya watoto katika nchi barani  Amerika ya Kusini, Afrika,Ulaya, Asia ya Kusini, Caribien na nchi za Mashariki ya Kati.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.