2017-05-10 15:07:00

Zaidi ya watoto 4,000 wamepoteza maisha kwa njia ya Boko Haram!


Matendo ya kigaidi ya Kikundi cha Boko Haram tangu mwaka 2014 kimeshambulia zaidi watoto. Watoto wengi wanatumiwa kama mashumbulizi ya kujitoa muhanga.Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Sekretarieti Kuu ya Umoja wa Mataifa juu  ya watoto na migogoro ya silaha kwa mwaka 2013 -2016 , inaonesha watoto wanazidi kuteseka kiukatili katika mikono ya magaidi wa Boko Haram katika eneo la Kaskazini mwa Nigeria.
Taarifa inasema; kwa miaka mitatu wameua watoto zaidi ya 4,000 na 1,650  kufundishwa kushika silaha au kuingizwa katika kundi lao. Aidha mashambulizi dhidi ya jamii na mapigano dhidi ya vyombo vya usalama vimeacha ulemavu wa viuongo kwa watoto 7,300. Katika ripoti ya Umoja wa Mataifa pia inaonekana wazi kwamba  kulipuka kwa mabomu ya kuua  ndiyo sababu ya pili ya vifo miongoni mwa watoto.

Baadhi ya shuhuda mbalimbali zilizotolea na watoto wadogo waliokombolewa, wanasema, wengi wao wanatekwa lakini wengine ni kwasababu ya uchumi au shinikizo la familia. Hiyo imetokana na wakati mwingine wazazi wenyewe hutoa watoto wao ili wapate ulinzi  au faida kiuchumi.
Mashule ndiyo lengo kuu la mashambulizi ya kigaidi, kwani kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, inaonesha kwamba ni takribani ya mashule 1,500 yaliyo haribiwa kwa mwaka 2014 na rekodi za waathrika ni  1280 katika ya wanafunzi na walimu wao. Tangu mwaka 2014 ni zaidi ya 4000 ya watoto ambao wameteswa,au kulazimishwa kuolewa na pia kubadilisha dini kuwa waislam.

Aidha,kundi la wataalam wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa wamekaribisha tarehe 9 Aprili 2017  kuachiwa huru kwa wasichana 82 wa Chibok waliokuwa mikononi mwa Boko Haram, na kutoa wito kwa serikali ya Nigeria na jamii ya kimataifa zichukue hatua zote stahiki kuhakikisha kuwa wote waliokamatwa na Boko Haram wanaachiwa huru.
Wataalam hao ni Maud de Boer-Buquicchio,mhusika na uuzaji wa watoto, Urmila Bhoola muhusika na utumwa, na Dainius Pûras muhusika na haki ya kuwa na afya bora. Halikadhali wanatoa wito ili  wasichana walioachiwa huru wapewe msaada utakaowawezesha kujiunga tena na jamii zao na kuishi maisha ya kawaida, huku haki zao zikiheshimiwa kikamilifu.Hiyo ni pia inajieleza wasiwasi mkubwa uliopo kuhusu hatma ya wasichana zaidi ya 100 ambao bado wanashikiliwa na Boko Haram, pamoja na familia za wasichana hao. Ikumbkwe tarehe 14 Aprili 2014 kikundi cha kigaidi cha Boko Haram kiliivamia shule ya Chibok Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na kuwateka nyara wanafunzi 276.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.