2017-05-10 13:45:00

Kard.Montenegro:Maskini wote ni sura ya Kristo tusifanye ubaguzi


Hata miongoni mwa Wakristo leo hii kumeenea falsafa fulani ya kutoa upendo ambao kila mmoja anamua ni  masikini gani anapenda kumsaidia bila kuwa na aibu ya wengine; wanasahau kuwa kila mmoja wao ni Kristo. Na hivyo tunaomba kwa bidii zote Bwana wetu Yesu Kristo wakati huo hatujisikii wadhambi wa kumfukuza kwa mfano mkimbizi, muhamiaji au mgeni kwasababu wote tunawaona ni magaidi au kuwadhania ni wabaya. 
Haya ni maeno makali na  maonyo ya Kardinali Francesco Montenegro wa Jimbo Kuu la Agrigento nchini Italia wakati wa mahubiri yake akiongoza Misa Takatifu tarehe 8 Mei 2018  mbele ya uwanja  wa Madhabahu ya Mama Maria wa Rosari mjini Pompei, kama utamaduni kwa siku ya tarehe 8 Mei ya kila mwaka Kanisa katoliki linafanya ibada ya kuheshimu Mama Maria wa Rosari wa Pompei.

Uwanja ukiwa umefurika waamini na mahujaji wengi kutoka Mkoa wa Campagna,na mikoa mingine ya Italia wakiwemo hata  wageni kutoka nchi za, Askofu Mkuu wa Agrigento ambaye pia ni Rais wa Caritas nchini Italia baada ya maadhimisho ya misa aliongoza sala ya Mama Maria iliyotungwa mwaka 1883 na mwenye Heri Bartolo Longo mwanzilishi na mfadhili wa madhabu hiyo.  Bartolo Longo alizaliwa tarehe 11 Februari 1841 na kifo chake huko  Pompei tarehe 5 Oktoba 1926, akatangazwa mwenye Heri na Mtakatifu Yoane Paulo II tarehe 26 Oktoba 1980.

Askofu Mkuu Montenegro katika mahubiri yake amesema upendo ni kama kipima joto  cha imani ambapo upendo wa kweli hautakabali bali ujazwa na ishara kamili. Imani inayotazama juu ya hanga tu na  kasahau kuchungulia chini ya ardhi imekufa. Kwasababu Bwana anahitaji kuona matendo halisi na ya kweli,yenye uwezo wa  kutambua hali halisi na mahitaji ya wadhaifi, kuwasaidia wale wasio kuwa na makazi au bila mkate wa kula, awe ni mzalendo na hata mkimbizi na muhamiaji bila ubaguzi wowote.

Akikimbusha juu ya aina nyingi za umaskini na machafuko ya kijamii yaliyoko njchi Italia :Kardinali Montengro anasema nchini Italia chakula kinachotupwa ni kiasi cha bilioni 8.7, wakati huo kila mara unakumbana na watu wasio kuwa na chakula wakilazimika wengine kwenda kwenye mapipa ya takataka. Kwa njia hiyo natoa wito wa kutokuwa tofauti mbele ya kilio cha ndugu wanao endelea na mateso hayo. Hiyo ni kwasababu anasema, matendo ya upendo ni lazima yatoe msukumo wa nje, kwenda kukutana watu,kuwasaidia wengine na kuwashirikisha kile tulicho nacho kama zawadi tunayoipata kila siku kutka kwa Mungu, ili hawa wasijisikie wapweke wa kutelekezwa na jamii na kukosa matumaini.

Naye Askofu Mkuu Tommas Caputo  Msimamizi wa Kitume wa Madhabau ya Pompei wakati wa kumkaribisha Askofu Mkuu Montenegro amekumbusha wamini wote  juu ya kuanza kwa upya Pompei katika uotoaji wa huduma na kwamba huduma za kijamii ziweze kuchanua na zaidi kutoa kipaumbele cha maskini katika kuwarudishia adhi ya utu wale wanaohitaji maana ni mfano wa sura ya Kristo Yesu. Ikimbukwe  Askofu Mkuu Tommas Caputo,tangu 1993 hadi 2007 aliwahi kuwa Mkuu wa Protokali katika ofisi za Katibu Mkuu wa Vatican, wakati huo huo mwaka 2007 akateuliwa kuwa Askofu Mkuu na Balozi wa Kitume wa Papa katika Kisiwa cha Malta na Libia Afrika.

Mwaka 2011 alitoa wito kwa serikali za mataifa waweze kujihusisha na uokoaji wa wakimbizi kutoka Eritrea kuelekea Libia na pia kuwapokea wahamiaji wote. Mwaka 2012 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteua kuwa msimamizi wa kitume katika madhabau ya Kipapa ya Bikira Maria wa Rosari katika mjini ajulikanao kote ulimwenguni Pompei.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.