2017-05-07 12:26:00

Papa: Shahada hazisaidii kitu kama kuhani hajui kubeba Msalaba!


Ndugu zangu watoto wetu wameitwa katika daraja la upadri. Hebu tutafakari juu utume wao wa Kanisa  watakao tenda. Kama mjuavyo Bwana Yesu Kristo di kuhani mkuu wa Agano jipya, lakini kwa njia yake watu wote  watakatifu  wa Mungu wamekuwa kuhani. Hata hivyo kati ya wafuasi wake wote, Bwana Yesu anataka kuchagua wachache ili waweze kutumikia hadharani katika Kanisa kwa jina lake maalumu la kikuhani kwa ajili ya watu wote na utume wake uweze kuendelea kama Mwalimu, kuhani na mchungaji. Hawa wamechaguliwa na Bwana siyo kwa ajili ya kazi bali kwa ajili ya kutoa huduma.

Ni maneno ya mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko  tarehe 7 Aprili 2017 wakati Kanisa linaadhimisha Jumapili ya Kristo Mchungaji mwema, inayokwenda sambamba na Siku ya 54 ya kuombea Miito Duniani, ambapo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu ametoa Daraja la Upadre kwa Mashemasi 10 kutoka jimbo kuu la Roma.

Baba Mtakatifu Franciko anasema ,kama Yesu alivyo kuwa ametumwa na Baba yake, hivyo kwa mara nyingine tena anawatuma mitume kwanza na baadaye Maaskofu na wafuasi wake, hatmaye wanaongezeka washiriki ambao ni makuhani  ili kuungana pamoja katika huduma ya kikuhani .Kuhani anaitwa kutoa huduma kwa watu wa Mungu. Baada ya tafakari na maombi , vijana  hawa kwa utaratibu watapewa daraja la upadre ili wawe wahudumu wa Kristo, Mwalimu , kuhani na mchungaji,waweze kufanya utume kwa pamoja katika kujenga mwili wa Kristo ambao ni Kanisa la Mungu  na Hekalu la Roho Mtakatifu. Wao watakuwa wamefanana na Kristo kuhani Mkuu , kwani watawekwa  wakfu kama kweli Kuhani wa Agano jipya, na kwamba,wasifu huo unawaunganisha katika ukuhani na Askofu ,watahubiri Injili , watakuwa wachungaji wa watu wa Mungu  na kuendesha shughuli zote za kuabudu hasa katika maadhimisho ya sadaka ya Bwana.

Baba Mtakatatifu Francisko akiwageukia mashemasi ,amesema wafikirie: kwa kutoa huduma ya mafundisho Matakatifu ya Mungu ,watashiriki katika huduma ya Kristo ambaye ni Mwalimu pekee. Anaongeza; jikiteni kwa undani katika Neno la Mungu ambalo ninyi mlipokea kwa furaha. Someni na kutafakari kwa juhudi Neno la Bwana na kuamini kile mlichosoma, kufundisha kile mlichojifunza kwa imani, na kuishi kwa imani kile mlichofundisha. Amewashauri ; msifanye mahubiri marefu ya kiakili na kisomi, ongeeni kirahisi kutoka moyoni, na mahubiri hayo yatakuwa ya kweli na kiungo.!
Aidha Mafundisho yenu yawe chakula kwa watu wa Mungu, na harufu nzuri ya maisha yenu iwe ni furaha na msaada kwa watu wa Kristo kwani kwa njia ya maneno na matendo yenu, yaweze kijenga nyumba ya Mungu ambayo ni Kanisa. Anatoa mfano kwamba, maneno bila mifano ya maisha hayasaidii kitu, bora kurudi nyuma. Na maisha ya kinafiki ni ugonjwa mbaya katika Kanisa.

Ninyi muendelee na kazi ya utakaso wa Kristo, ni kwa njia ya huduma na  sadaka ya kiroho ambayo uwakamilisha waamini, kwasababu ni kuunganisha dhabihu ya Kristo kwa njia ya mikono yenu kwa jina la Kanisa, ambapo utolewa kwa kwa njia ya umwagaji damu madhabahuni  wakati wa maadhimisho ya mafumbo matakatifu. Hivyo Baba Mtakatifu anasisitiza kwamba,mtambue kile mnachotenda. Igeni kile mnacho adhimisha kwasababu katika kushiriki fumbo la Kifo na ufufuko wa Bwana, mnabeba  kifo chake Kristo katika miili yenu na kutembea naye katika upya wa maisha.Anatoa mfano ,Kuhani aliyesoma labda taalimungu nyingi na akawa na shahada moja mbili  tatu lakini hakujifunza  kubeba msalaba wa Kristo , hasaidii . Anaweza kuwa na taaluma na ni  profesa mzuri lakini siyo kuhani.

Katika ubatizo mnaungnisha watu wengi wapya kwa Mungu. Katika sakramenti ya kitubio mtasamehe dhambi kwa jina la Kristo na Kanisa. Tafadhali ninawaomba kwa jina la Kristo na la kanisa muwe wenye huruma daima.Msiwabebeshe waamni mizigo mizito ambayo haweze kubeba na hata ninyi pia.Yesu mwenyewe aliwakaripia walimu wa sheria na kuwaita wanafiki. Katika mafuta ya wakfu mtawapaka wagojwa. Ni moja ya kazi labda inayoleta uvivu na ya uchungu,lakini manapaswa kwenda kuwatembelea wagonjwa , Baba Mtakatifu anasistiza , nendeni ninyi wenyewe, kwasababu ndiyo mara nyingine wanakwenda waaminii walei na mashemasi , lakini hata ninyi pia msiache kuguswa na nyama ya Kristo mteseka katika wagonjwa. Hawa wanawatakatifuza ninyi wanafanya mkribie Kristo. Katika kuadhimisa ibada mbalimbali za siku kama vile masifu ya  asubuhi, jioni, sifa na maombi mtakuwa mnawakilisha sauti ya watu wa Mungu na binadamu wote.

Katika utambuzi wa kuchaguliwa katika wanadamu na ili kufanya mambo ya mungu, lazima mjikite katika shughuli ya furaha na upendo wa kweli, katika huduma ya Kristo . Muwe na furaha daima, toeni furaha ya huduma ya Kristo hata katikati ya mateso, kinzani na dhambi binafsi.
Daima mbele yenu uwepo mfano wa mchungaji mwema aliyekuja kwa jili ya kutumikia na siyo kutumikiwa. Tafadhali msiwe mabwana na hata kama watumishi wa serikali bali wachungaji : wachungaji wa watu wa Mungu kwa lengo la ufalme wa Mungu na siyo kwa lengo binafsi.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.