2017-05-06 14:54:00

Vijana mliochagua njia ya kumfuasa Kristo toa huduma kwa maskini!


Jumamosi 6 Mei 2017 Baba Mtakatifu Francisko amekuta na kuongea na Jumuiya ya Seminari ya Kipapa Campano nchini Italia , wakisindikizwa na Baadhi ya Maaskofu wa Mkoa. Ameshukuru uwepo wao wote na hasa maneno ya Gombera katika hotuba yake na kushukuru kwa idadi kubwa ya waseminari hiyo ya Kipapa. Seminari yenu inawakilisha historia ya aina yake katika  Kanisa la Italia. Ilianzishwa  mwaka 1922 kwa matashi ya Papa Pius X, na kama ilivyokuwa kawaida  wakati huo Taasisi nyingi za mafunzo zilikabidhiwa katika maongozi ya Mapadri wa Kijesuiti. Katika mongozi yao kwa miaka mingi wameweza kuleta mabadiliko mengi na pia kuendelea kuongoza Seminari hiyo. Kwa miaka ya karibuni umeongezeka ushirikiano na makanisa mengine ya majimbo lakini pamoja na majimbo hayo kutuma vijana wao, wamejikita katika ugunduzi wa mapadri wanaostahili kuongoza mafunzo ya vijana hao.

Baba Mtakatifu anawatia moyo katika safari hiyo muhimu ambayo inatoa matunda ya umoja wa Kanisa, ambapo majimbo mahalia na wachungaji wake wako wanawekeza rasimalai kubwa. Anasema muungano wa Majimbo ya kuwaandaa vijana katika mafundisho ya kikuhani  yanawakilisha bila shaka fursa na utajiri, kwa njia ya karama mbalimbali na uzoefu wa kila mmoja ambapo kila mmoja anautoa katika mafunzo ya  mapadre endelevu katika umoja wa Kanisa la Kristo. Hiyo ni pamoja na kupanua upeo wa kuota ndoto ya wito, kwa urithi  wa roho ya kimisionari (Ratio fundamentalis institutionis sacerdotalis, 9) ambapo siyo kusema ni  udhaifu  bali ni kuimarisha na kutoa maana ya kushiriki katika msingi wa Kanisa mahalia.Katika kipindi ambacho wote tunajisia wadhaifu na hiyo ni kutokana na wasiwasi wa changamoto zilizoko mbele kwa upande wa mafunzo,jambo msingi ni kutembea pamoja na roho ya pamoja. Baba Mtakatifu anasema  ndiyo njia pekee ya kushinda kwa  kujisia kusaidiwa,kuhamasika na kutajirishana na wengine. Mazoezi hayo ya umoja yanatokana na utajiri wa kukutana na utamaduni wa kiroho katika maongozi ya mafundisho ya Kijesuiti; kwa njia ya mafungo ya kijesuiti katika mafunzo yenu yote kwa hakika ni mwongozo wa mafundisho ya Kanisa.

Baba Mtakatifu akuwageukia wakufunzi wao, anasema wafundishe katika roho ya upadre kwa njia ya mafundisho ya Mtakatifu Ignatius , huo ndiyo utume wenu, ni changamoto lakini wakati huo ni sifa  kuelekeza vijana katika maisha elendelevu ya utume wa ukuhani. Anaelekeza  mambo matatu  muhimu ya kuelimisha, kwamba  kuelimisha katika mtindo wa Iginatius maana yake ni kusaidia mtu ajitambua yeye mwenyewe hasa msingi na mahusiano yake na Bwana Yesu. Hiyo ndiyo shemu ya kwanza  na ya kina ya uhusiano wa Bwana aliye waita marafiki (Yh 15,15) .
Kwa njia hiyo ni muhimu kutambua, kupokea na kufundisha daima utu binafsi. Mwongozo huo  pamoja na mafunzo ya kiakili hayana maana ya kujifunza na baadaye kutoa huduma tu bali ni kusaidia kuchota zana nyeti kwa mantiki halisi ya kujitambua binafsi  kwa mfano wa  ( wewe ndiye Kristo, wewe ndiye Petro (Mt 16,16.18): kujikita katika safari ya wito kama vile Mtakatifu Petro mtume , safari hiyo  inazunguka katuika mazungumzo ya upendo na  urafiki na zaidi iwapo  utakuwa umetambua  kuwaYesu Masiha ni  Bwana wa amaisha yetu, ni yeye nayetupatia jina linalojikita katika wito wetu, na kutoa utambulisho wa utume wetu ambao Mungu anautambua na kuutunza daima.

Ugunduzi wa jina jipya, jina dhahiri Baba mtakaifu anasema, linajieleze kwa njia ya uwezo wa kutoa  jina katokana na uzoefu mbalimbali wa ubinadamu wetu. Kuita vitu kwa jina ni hatua moja ya utambuzi  wa mapenzi ya Mungu katika maisha yetu. Baba Mtakatifu anawaalika waseminari wasiwe  na hofu kutoa majina kutazama bayana ukweli wa maisha yao ili kujifungua wazi kwa wengine, zaidi wakufunzi wao ili kuweza kushinda  vishawishi vya kuishi ukuhani kama desturi sababu ni desturi na siyo kutoka moyoni. Mang’amuzi ndiyo ushauri wa pili wa kusisitiza: Mafundisho juu ya mang’amuzi Baba Mtakatifu nasema haupo katika mtindo wa Kijesuiti  lakini ni hatua ya nguvu. Kipindi cha kuwa seminari ni cha mang’amuzi kwa neema ya kusindikizwa kama vile  Mzee Eli alivyo msindikiza Samueli (1Sam 3). Wasindikizaji wanasaidia vijana kutofautisha  sauti ya Bwana na sauti nyingine zinazotokea huku  na kule katika masikio na mioyo yao.  Lakini wakati huo , mang’amuzi yanapaswa kusaidiwa kama sanaa ya kweli ya mafunzo kwasababu kuhani lazima awe kweli mtu wa mang’amuzi. ( Taz.Ratio fundamentalis, 43).

Leo hi ina zaidi Kuhani anaitwa kuongoza wakristo wote katika mang’amuzi ya ishara ya nyakati na katika kutambua sauti ya Mungu kati ya sauti nyingi zinazojitokeza ili kuweza kufanya mang’amuzi binafsi kwenye  hofu za ndani binafsi. Ili kuwa waamini  wa mang’amuzi  lazima kuwa wajasiri; mang’amuzi yanahitaji ujasiri tofauti na kuishi njia rahisi.Hii ni mifano ambayo mara nyingi amekuwa anaelezea Baba Mtakatifu.
Kufundisha namna ya kung’amua maana yake ni kuondokana na vishawishi vya kutaka kurudi nyuma au kuwa na desturi za ugumu pia uhuru wa kufikirika. Kufundisha namna ya kung’amua maana yake ni kutaka kuondokana na malimwengu, au kuhukumu ili kujifungua uwazi, kumwachia nafasi Mungu aongee ndani ya moyo leo hii katika ulimwengu wa sasa mahali ulipo. Baba Mtakatifu anaelezea aina ya tatu ya  kujifunza ukuhani kwa njia ya mtindo wa mtakatifu Ignatius akisema, maana yake ni kufungua upeo mkubwa wa Ufalme wa Mungu kwa kuongozwa na shauku kubwa ya ukarimu wa kutoa maisha kwa Bwana na ndugu. Kwa njia hiyo mmechagua mada isemayo tafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake (Mt 6,36):mada hiyo itawasaidia kupanua mafunzo yenu ,ambapo msiridhike tu kufikia lengo la kuvaa mavazi ya makasisi, itawasaidia kutokuwana haraka ya kumalizia safari yenu tu bali kuwahimarisha katika muundo wa kibinadamu na kiroho.

Kutafuta ufalme wa mungu inasaidia kuendeleza kile ambacho mmekwisha pokea katika kutafuta utakatifu kwa njia ya kutoa huduma kwa Mungu na ndugu. Kutafuta ufalme wa Mungu maana yake ni kutafuta haki ya Mungu na kutenda kazi yake ili mahusiano ya kijumuiya na miji yaweze kugeuka upendo wa uhuruma ya Mungu anayesikiliza kilio cha maskini. Kutafuta haki ya kweli inasaidia kukuza uhuru wa ndani ili kutambua mambo mengi ya dunia hii hata wito wenyewe. Vijana wengi waliochagua kumfuata Bwana katika njia ya ukuhani wanaitwa kukuza urafiki na Bwana Yesu anayejionesha kwa njia ya wapendwa wake ambao ni maskini, kuwa shahidi wa umaskini kwa njia ya ujasiri wa maisha, kuwa mfano hai wa kuhamasisha haki ya kijamii.
Kwa maombezi Maria Malkia wa Mitume na Mtakatifu Alfonsi Maria wa Liguori na Mtakatifu Iginatius mwalimu wa Mang’amuzi, Bwana awasaidie kuendele akwa furaha na uaminifu  njia inayong'aa  tamaduni mnazotokea!

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.