2017-05-06 14:17:00

Papa akutana na Wanajeshi wapya wa Kikosi cha Ulinzi wa Vatican!


Baba Mtakatifu  Francisko Jumamosi 6 mei 2017 amekutana Wanajeshi wapya 40 wa Kikosi cha Ulinzi na Usalama cha Vatican wakiwa wanasheherekea kuhitimu mafunzo yao katika mfumo mpya wa Vatican. Wanajeshi wa Uswis pia  wanafanya kumbu kumbu ya Maaskari 147 kutoka Uswis waliofariki dunia tarehe 6 Mei mwaka 1527 dhidi ya wanajeshi wa Ujermani chini ya utawala wa Carlo  V wa Asburg. Ni miaka 490 iliyopita wanajeshi walitoa maisha yao kumlinda Khalifa wa Mtume Petro. Baba Mtakatifu anasema, anayofuraha ya kukutana nao katika siku hiyo na  kuwapongeza  wahitimu  waliochagua kwa miaka ya ujana wao kutoa  huduma kwa khalifa wa mtume wa Mtakatifu Petro. Anasema uwepo wa wazazi,ndugu na marafiki Roma kusheherekea na nyinyi katika sikukuu ni kuonesha  ukarimu wa wakatoliki wa Uswis Vatican pia mafundisho ya kikristo ambayo ni mifano mizuri ya imani ya wazazi walioonesha watoto wao hata thamani ya kushiriki katika jumuiya ya kikristo katika maana ya kutoa  huduma ya Kanisa.

Kila mwaka mnafanya kumbukumbu ya uchungu, wakati huo huo ni maarufu ya (Sacco di Roma), katika kutoa heshima katika  mnara wa mashujaa wa Askari  kutoka Uswiss waliotoa sadaka ya maisha yao  kwa ujasiri wakati wa kumlinda Khalifa wa Mtakatifu Petro. Leo hamwalikwi kuwa mashujaa wa kutoa maisha kimwili, bali katika kutoa sadaka kubwa ya huduma  kwa nguvu ya imani. Imani ina nguvu ya kushinda aina zote za nguvu za ulimwengu huu na zaidi mtawala wa nchi hii, ibilisi wa uongo kama asemavyo Mtakatifu Petro “maana adui yenu, ibilisi huzunguka zunguka kama simba angurumaye akitafuta mawindo”(1Pt 5,8).

Mnaalikwa kuwa nguvu na thamani muhimu kwa msaada wa imani katika Kristo na katika neno lake la uokovu. Uwepo wenu katika Kanisa na  huduma yenu muhimu Vatican ni fursa ya kukua kwa ujasiri kuwa wanajeshi wa Kristo. Mahujaji na  waamini wenye kubahatika kukutana na nyinyi,wanajengwa na kugundua ndani mwenu ile tabia yenu ya ukakamavu, utanashati, uwajibikaji kitaalamu na pia ushuhuda wa  ukarimu wa kikristo na maisha ya utakatifu.
Baba Mtakatifu anawaalika kwamba kwa kipindi wanachoishi mji huu wawe wazi kindugu,katika kushirikiana kusaidia wengine, kuwaongozo katika mfano wa kuigwa wa kikristo, huduma yao wanayotoa iongozwe na imani yao .Na kwamna hiyo ni imani yake kwamba msukumo wa nguvu ulio wafanya waje Roma kwa ajili ya kutoa huduma umetokana kwa dhati na imani yao.Utume mmoja waliokabidhiwa kwa niaba ya Vatican na Kanisa, chanzo chake ni ubatizo unao wawezesha kutoa ushuhuda wa imani katika Kristo aliyekufana na kufufuka na mahali ambapo neema ya Mungu inawaweka muishi.

Aidha anasema wajisikie kuwa sehemu ya watu wengi duniani wakiwa ni mitume na wamisionari wanaojikita kushuhudia Injili mahali ambpo wanatoa huduma,hata nje . Hiyo ni kwasababu inajikita katika ishara ndogo ndogo za kila siku, wakati mwingine  ni marudio, lakini ni muhimu kutoa huduma hiyo daima. Kwa namna moja au  nyingine ni mtindo wa maisha kimwili, kwasababuya ya ushirikiano na wengine katika umoja na wakubwa wenu, na kwa nje unaojionesha kukaribisha,upole na uvumilivu. Anawatakia mema ya kuweza kuhamasisha na kutoa thamani katika kipindi cha maisha yao kutokana na fursa za kukuza roho na utamani watakazochota Roma.Baba Mtaktifu anasema, Mtakatifu Filipo Neri ambaye kumbu kumbu yake ni  mwisho wa mwezi huu,alikuwa akiwasindikiza vijana kugundua mambo ya kale yamayohusu jumuiya ya wakristo wa zamani yaani  njia ya watakatifu. Hiyo ni hoja kubwa kwenu ya kufanya ya kupitia  njia ya watakatifu Roma walioishi katika mji huu. Na hiyo ndiyo itakuwa tunu msingi isiyo sahaulika na tajiri katika muda wa kuishi Roma.

Anachukua fursa hiyo kwa ajili ya kurudia upya kuwakushukuru  wanajeshi wote wa Kikosi cha Ulinzi wa Uswis, kwamba anatambua shughuli yao stadi na thamani kubwa kwa ajili huduma ya papa na kwa mji mzima wa Vatican. Anamaliza akiwaomba sala kwa ajili yake  wakati akiwatakia matashi mema kwa njia ya Bikira Maria na wasimamizi wao Mtakati Martino, Sebastiano na Nicola wa Flue.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.