2017-05-06 11:47:00

Askofu mkuu Francisco Padilla ateuliwa kuwa Balozi nchini Qatar


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Francisco Montecillo Padilla kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Qatar. Ataendelea kuwa Balozi wa Vatican nchini Kuwait, Yemen, Bahrein na kwenye Nchi za Falme za Kiarabu. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Francisco Padilla aliwahi kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Tanzania. Askofu mkuu Francisco Montecillo Padilla alizaliwa kunako tarehe 17 Septemba 1953 Jijini Cebu, Ufilippini. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 21 Oktoba 1976. Tarehe 1 Aprili 2006 akateuliwa kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Papua New Guinea na Visiwa vya Solomon. Tarehe 23 Mei 2006 akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu. Tarehe 10 Novemba 2011 akateuliwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI kuwa Balozi wa Vatican nchini Tanzania!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.