2017-05-05 16:41:00

Papa: Iwapo matumaini ni hai utaona hata yale yaliyofichika!


Katika kilele cha kuadhimisha miaka 80 ya kuanzishwa kwa Taasisi ya Kipapa ya Kanisa la Romania mjini Roma , Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wanachuo na kutoa hotuba yake tarehe 5 Mei 2017 kwa ajili ya kuwatakia heri. Katika hotuba hiyo anasema, anayo furaha ya kuwasalimia wakati wanafanya kumbukumbu hiyo ambayo ni fursa ya kumshukuru Mwenyezi Mungu  pia wote ambao kwa miaka hii wamejikita katika juhudi zao kwenye Taasisi ya Pio Romeno katika mchango wao wa kutoa mafunzo kwa makleli wa maisha endelevu. Njia yao wanayoifanya ni sehemu  inayojikita katika historia iliyoendelea,  ambayo ni matokeo  ya badaye kwa ajili ya Makanisa ya Kigiriki na wakatoliki wa Romania. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko anawatakia heri ya mambo mawili kwanza kutunza kumbukumbu na kukuza  matumaini.

Katika kufafanua maana ya kutunza kumbukumbu anasema,Taasisi hiyo imetokana na na uwepo wa muda mrefu jumuia ya wakatoliki wa mashariki, na pia kuguswa kwa undani juu ya matukio ya kusikitisha zaidi yanayohusu utesi wa Kanisa ,ambapo  kwa miaka ya  karibuni wamejifungua zaidi katika kukabiliana na changamoto. Katika historia  hiyo imeunda mashahidi wengi wa Imani katika kipindi kigumu cha majaribu, kipindi cha giza na cha mwanga ambapo matukio yote haya yanawagusa ninyi kwa karibu. Kwa njia hiyo ni vema kutunza kumbukumbu, lakini msikubali kukandamizwa na kushikiria nyakati za nyuma ni lazima kuishi matukio  katika wakati uliopo.Hiyo ni  kwa msaada wa Injili iliyo hai, ambayo inakumbatia historia kubwa zaidi ya maisha yenu, pia jifungue wazi kwake Roho Mtakatifu. Iwe tunu kwenu kwa njia ya sala na masomo ya kina, ambayo Bwana alifunua kazi kubwa kwa njia ya watu wake kwasababu hiyo ni fursa kubwa kwa miaka mnayoishi Roma , maana mnaweza kupunua hali ya umoja wa Kanisa.

Katika kuhimarisha kumbukumbu ya Kanisa , mtasaidiwa kushinda majaribu ya hatari ambayo yanaweza kuonekana katika mambo yasiyo kuwa na maana  hasa katika  kufurahia maisha ya kawaida , mahali ambapo kila kitu kinaelendelea mbele  bila kuwa na shahuku wala harufu hatimaye mnaishia kuwa walezi wenye wivu na wavivu ambao wanashikiria kulinda usalama na ustawi binafsi.
Kwa njia ya mifano  hai ya kuonja zawadi ya injili, kuweni wachungaji  ambapo kila mchungaji anafananishwa na Kristo aliyetoa maisha yake na kuwapenda mpaka mwisho(Yh 13,1). Haiwezekani kabisa kushuka kwa kujikita  katika mambo yasiyo stahili na bila kujihatarisha. Daima Taasisi hiyo iwe kama uwanja wa kafanya mazoezi ya kutoa maisha katika uwajibikajii wa masomo yenu ambayo ndiyo zana za huduma kwa kanisa. Ni tajiri kwa ajili ya utamaduni wa nchi yenu, ambao lazima kutunza kumbukumbu, ambayo siyo tu kufikiria mambo yaliyo pita bali kuishi kwa matumaini.

Baba Mtakatifu anaelezea  matashi mema ya pili, maana ya kukuza matumaini kwamba,kuna haja moja muhimu ya kukuza matumaini ya kikristo , matumaini yanayotoa mtazamo mpya, wenye uwezo wa kugunduua na kutazama mema, hata mahali ambapo kuna giza la ubaya.
Mtakatifu Ephraimu aliandika kuwa “iwapo matumaini ni hai katika mitazamo yetu, tutaona yale yaliyojificha”. Hata katika Kitabu cha Matendo ya mitume ambapo Liturgia ya Pasaka inatushauri,inaonesha jinsi gani Kanisa linaishi katika matumaini ya mfufuka,  kuishi katika sala, umoja na upendo .Haupotezi kamwe mtazamo na kutoa matumaini  hata mahali ambapo hawaeleweki na bila  kuwa na zana za kuwasadia. Roho Mtakatifu aongeze ndani yao shuhuku ya kutafuta na kuhamasika kwa moyo wote njia ya mapatano na umoja kati ya wakristo.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.