2017-05-05 17:12:00

Kard Sandri:Utume endelevu wa Kanisa unahitaji kushirikiana!


Kwa ajili ya tukio la Jubileo ya miaka miaka 100 ya Taasisi ya Kipapa ya Mashariki tarehe 4-5 umefanyika Mkutano kuhusu “utambulisho na utume endelevu, kati ya uliopita na uliopo.”Ni Taasisi iliyoanzishwa tarehe 15 Oktoba 1917 kwa matashi ya Papa Benedikto XV ambayo ina katiba ya mafunzo ya elimu ya juu kuhusu masuala ya nchi za Maknisa Katoliki ya Mshariki.Katika tukio hilo Kardinali Leonardo Sandri Rais wa Baraza la Kipapa wa Makanisa ya Mashariki ametoa hotuba yake anasema kila maadhimisha kama hayo ni zawadi, ni shughuli ya mwendelezo wa nyakati zijazo pamoja na ukweli kwamba ni katika kujikita kwenye  mambo mapya na yenye kuwa fursa mpya kwa njia ya watu. Mwanzo wa Taasisi ya Kipapa  haikuwa katika kituo hicho, bali kuanzia mwaka 1922 baada ya kukabidhiwa  Shirika la Yesu(SJ) ikaendelea katika njia kwa utambuzi ndani ya umbu la Kanisa Katoliki , utambulisho na wajibu wa nafasi ya  makanisa katoliki ya Mashariki.

Anakumbuka hatua muhimu zilizopigwa  kwa muhongo huu kama vile Waraka kuhusu  maelekezo ya Makanisa ya mashariki  (Orientalium dignitas Ecclesiarum) wa  Papa Leone XIII; Kuanzishwa kwa liturujia ya Kilatini  (praestantia ritus latini) na Papa Benedikto wa XIV  mihongo miwili kabla, kuunda kwa Taasisi ya Kipapa na Papa Bendikto wa XV mwaka  1917, Hati ya maelekezo ya Mtaguso II wa Vatican (Orientalium Ecclesiarum), Safari ndefu iliyopelekea kutangazwa Sheria za  Makanisa ya Mashariki 1990; Waraka kuhusu  Makanisa ya Mashariki  wa  Mtakatifu Yohane Paulo II mwaka 1995; na   Ujumbe wa Kipapa  kwa Makleli katika  Makanisa ya Mashariki (Pontificia praecepta de clero uxorato orientali)  iliyotolewa mwezi Juni 2014 wa  Baba Mtakatifu Francisko .

Kardinali Sandiri anasema, Mei Mosi  miaka mia moja iliyopita Papa Benedikto XV aliandika ujumbe wake kwamba,  kuanzishwa kwa Taasisi ambayo ni mojawapo ya taasisi za kipapa, itaonesha furaha kubwa ya kwamba Kanisa lake Yesu Kristo siyo tu kwa ajili ya ya Kilatino, Kigiriki, lugha za mashariki bali ni ya Kikatoliki, ambapo hakuna ubaguzi wowote kati ya watoto wake wawe wa kilatini, kigiriki na hata mataifa mengine kwa maana wote ni muhimu mbele ya Kituo hiki cha Kipapa. Tukiwa wa kweli kwa kutazama ujumbe huo anasema,tunaweza kusema kwamba  hatua muhimu zimepigwa kama vile matunda ya wanasheria lakini pia hatua nyingine zinapaswa kutimilizika. Kwa mfano ukifikiria nchi za mshariki, mbali na mambo ya masomo  wengi sasa wamefungua macho yao na kuona kwamba katika karne  kadhaa uwepo wa wakristo katika ardhi hizo  kwa bahati mbaya umeathiriwa  na ghasia za vita na kama vile Syria na Iraq. Pamoja hayo pia ni dhahiri kuona kwamba bado mashahidi wanaendelea, matukio ya hivi karibuni katika nchi za Misri, lakini pia mikutano ya kiekumene.

Kazi ya kushirikiana na Baraza la Kipapa kwa ajili Makanisa ya Mashariki kama ile ya mafunzo  katika chuo, inawezekana kwa sababu kila mmoja ameitwa kutoa jibu kila siku  ambapo ni lazima kujikita ndani ya safari ndefu ya Kanisa mchumba mwema  wa Kristo.
Kardinali Sandri anaendelea na hotuba yake, wakati mwingine hatutambui kwa haraka namna tulivyo wafumaji wazuri kuweza kukamilisha njia ambayo ni ya makutano, au kama mafundi wa kuweza kufuma kwa tararibu baadaye kutoa kifaa kilicho kizuri. Tatizo linatambulika tu pale unapoanza kulalamika kutokana na shughuli  unayokabiliana nayo. Kipindi cha mkutano kama hayo ni fursa kubwa ya kuweza kuamka na kutazama upeo mkubwa, ni lazima kujikita kwa undani kuona nyuso zote, kusikiliza na kutafakari na wengine hatua  ambazo taasisi zimepitia na kufikia kwa miaka yote hiyo. Kwa kutambua hivyo unaweza kuona wazi mapana na marefu zaidi ya taasisi ilivyo fanikiwa. Aida unaweza kundua kwamba Chuo hicho sasa ni mama wa dunia na siyo tu kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki bali kutoka hata katika makanisa mengi ya dunia kama vile Caucaso, Ulaya Mashariki, au Kerala  na India ya Kusini.

Aidha ameomba kukumbuka sura tatu ili zisaidie zaidi kupanua upeo wa nafasi ya hema kama asemavyo Nabii Isaya , hiyo ni kwasababu mtazamo mpana wa muhongo huu katika Taasisi ya Kipapa. Kwanza Patriaki  wa Kiekumene Bartholomew I alisomea katika Taasisi hiyo, mara nyingi amekumbuka chuo  na pia hiyo inadhihirisha juu ya urafiki  uliopo kati ya Baba Mtakatifu Francisko, kwa mkutoa mifano dhahiri, walivyokuwa pamoja katika Kaburi Takatifu Yerusalem, Katika Bustani ya Vatican waliposali pamoja kwa ajili ya nchi ya Israeli na Palestina, katika kisiwa cha Lesvos wakiwa na wakimbizi, na hata hivi karibuni Mjini Cairo katika Chuo Kikuu cha Al -Ahza, pia  katika kanisa kuu la Kiorthodox. 
Kumbukumbu ya Pili ni ile ya Mwenyeheri Vincenzo Eugenio Bossilkov , wa Shirika la Mateso na Askofu wa Nicopoli nchini Burgaria , ambaye ni shahidi wa imani katoliki dhidi ya wakomunisti. Naye alisoma katika Taaasisi hiyo, wanafunzi wengi wameweza kutumia maandishi yake katika masomo yao juu ya mateso ya Kristo  (studium Christi) na damu yake.

Na sura ya tatu ni Mwenye heri Alfredo Ildefons Schuster , ambaye alikuwa Gombera wa kwanza wa Taasisi ya Kipapa ya Mashariki. Yeye alikuwa ni mwanashirika wa Benediktini na mwanafunzi, baadaye akaitwa kuendelea na majukumu ya kichungaji katika Jimbo la watakatifu Amboros na Carlo huko Milano. Kwa njia hiyo Kwa maombezi yake awalinde mapadri wa kijesuiti, wakuu na wakufunzi ambao leo hii wana waandaa wengi watakao itwa kuwajibika katika makanisa ya kesho. Anamalizia, kama Baraza na kama Taasisi , pamoja na Baba Mtakatifu , tuendelee kutembea pamoja ili  kurudi katika chemichemi ambayo ndiyo mwanzo wa pamoja  kurudia safari yetu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.