2017-05-04 16:49:00

Tendo la Filipo kukaribia Towashi ni wito kwa Kanisa kusikiliza watu!


Kanisa liwe kidete na kutembea , kwa kusikiliza mahangaiko  ya watu na daima kuwa na furaha. Ni wito wa Baba Mtakatifu Francisko alio utoa katika mahubiri yake kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Marta Mjini Vatican Alhamis 4 Mei 2017. Katika sura nane mfululizo wa masomo kutoka katika kitabu cha matendo ya mitume , ni ufupisho wa historia nzima ya Kanisa. Ikiwa inaunganisha , mahubiri, ubatizo, uongofu , miujiza , mateso, furaha na hata ubaya wa dhambi kwa wale wanao karibia kufanya Kanisa kwa ajili ya kufanya biashara zao.Kwa maana ya wale wafadhili wa Kanisa ambao baadaye wanaibia kanisa akiwataja mfano wa Anania na Safira.

Pamoja na mahubiri hayo Baba Mtakatifu achambua Injili iliyosomwa, akisema kwamba Bwana alikuwa amewaeleza mitume wake tangu mwanzo ya kwamaba atawasindikiza kwa neno na ishara za miujiza  na kwamba hasinge waacha kamwe peke yao, na hata katika kipindi kigumu.
Baba Mtakatifu anatafakari maneno matatu, yaliyosomwa ya siku katika kitabu cha matendo ya mitume na kuwaalika watafakari kwa utulivu wakiwa nyumbani sehemu hiyo. Neno la kwanza ni kuamka na kwenda, kama ilivyosikika mazungumzo kati ya Malaika na Filipo. Hiyo ni ishara ya uinjilishaji anasema na kuongeza, wito ni kitulizo cha Kanisa kwa maana ni uinjishaji. 

Kwa njia ya kuinjilisha inabidi kwenda na siyo kubaki umekaa na utulivu nyumbani kwako , hapana! Ili Kanisa kuwa aminifu kwa Bwana daima linapaswa kusimama na kwenda. Kansa lisilosimama na kutembea likaugua. Kanisa hili linaishia kufungwa na mateso mengi ya kiroho na kisaikolijia, inafungwa na kujiingiza katika mambo madogo madogo  ya kidunia hasa masengenyo, inafungwa bila kuwa na upeo:na hivyo  amka ,simama na tembea ndivyo mambo yanayotakiwa Kanisa kufanya katika uinjilishaji. Songa mbele na ukaribie gari hilo, ndiyo wito alio pokea Filipo kutoka ndani ya Roho. Baba Mtaktifu anabainisha neno la Roho . Katika gari hilo kulikuwa na towashi wa mkushi akisoma maneno matakatifu wakati yuko njiani kuelekea kuabudu Mungu huko Yerusalem. Njiani alikuwa akisoma  sehemu ya Nabii Isaya; Baba Mtakatifu Francisko anasema hii ni kama kueleza uongofu wa aliyekuwa waziri wa uchumi  ambapo ni muujiza mkubwa. Tendo la  Roho Mtakatifu  kumshauri Filipo kumsogelea mtu yule , ya ni kuonesha   umuhimu wa  Kanisa jinsi ya kuwasikiliza wanye kuteseka katika mioyo ya kila mtu.

Watu wote wana mahangaiko ya mioyo  kwa wema na ubaya, lakini kuna mahangaiko. Inabidi kusikiliza haya mahangaiko. Hiyo kwasababu Roho haikumtuma Filipo  aende kufanya propaganda! Ilimtuma aende kusikiliza. Kwa njia hiyo kisikiliza ni hatua ya pili; ya kwanza amka na simama na ya pili sikiliza. Kwa maana ya uwezo wa kusikiliza watu wanafikiria nini na wanajisikia nini ndani ya mioyo yao mahali ambapo wamejaa mahangaiko. Hata kama wanafikiria makosa,lakini ni muhimu kuwasikiliza na kutambua mahangaiko yao ndani ya roho zao.Baba Mtaktifu Francisko ansisitiza kuwa hatua ya pili ya Kanisa linapswa kwenda kukutana na watu wenye kuwa na mahangaiko. Towashi  mwenyewe baada ya kumwona Filipo anamkaribia aliulizia kwamba Nabii Isaya alikuwa akisimulia juu ya nani na kumkaribisha apande katika gari lake. Kwa unyenyekevu, Filipo alinaza kuhubiri. Baba Mtaktifu Franciko akongeza kusema, mahangaiko ya mtu huo yakapaya maelezo ambayo yalimjaza matumaini ya moyo wake.Lakini yote hayo yaliwezekana kutokana na kwana Filipo alimkaribia na kumsikiliza. 

Wakati Towashi anasikiliza, Bwana alikuwa anafanya kazi ndani yake.Kwa maana hiyo Mtu huyo alitambua kwamba Nabii Isaya alikuwa akielezea Yesu. Imani yake kwa Yesu ikaongezea hadi walipokaribia mahali penya maji , akaomba kubatizwa.Ni yeye mwenyewe aliyeomba ubatizo kwasababu Roho alikuwa amefanya kazi katika moyo wake. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko anatoa wito ya kwamba, ni vema kuacha roho mtakatifu afanya kazi yake. Baada ya ubatizo Roho Mtakatifu anaendelea kufanya kazi daima maana anamchukua Filipo sehemu nyingine, wakati huo Towashi amejaa furaha na kuendelea na njia yake. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko anaonesha neno la tatu kwamba ni furaha yaani furaha ya kikristo.

Anamaliza mahubiri yake akitoa wito wa Kanisa lote kusimama kwenda, kuwa mama anayesikiliza, kwa neema ya Roho Mtakatifu anayeshauri neno la kusema. Mama Kanisa  anatoa mwanga kwa watoto wake ni maneno gani ya kusema na siyo maneno yanayofanya propaganda, bali ni kwa njia  ya kutoa ushuhuda wa utiii. Leo hii Yesu anasema kwa njia ya Kanisa kuweni na furaha kwa maana wakristo wote mmetawanyika popote duniani. 

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.