2017-05-04 17:13:00

Maaskofu wa Cuba wakutana na Baba Mtakatifu katika ziara yao !


Baba Mtakatifu amekutana na maaskofu wa Cuba na kuzungumza nao kuhusu Kanisa la Cuba, ambapo maaskofu hawa wako katika ziara ya kitume na Baba Mtakatifu  tangu tarehe 25 Aprili hadi 4 Mei 2017. Unjilishaji ulianza  mwaka 1494 mara bada ya kufika wahispania. Ilikuwa miaka miwili baada ya kufika Chritopher Kolumbus tarehe 13 Juni 1494 , ambapo padre Juan Solorzano aliadhimisha misa ya kwanza kando kando ya mto Jatibonico.

Vatican ilimtuma mwakilishi wake wa kwanza wa kitume huko Cuba Monsinyo  Plácide-Luis Chapelle (1898-1905); na tarehe 10 Mei 1916 Baba Mtakatifu Benedikto XV akatangaza Mama Maria wa upendo  Cobre ( anayeitwa kwa jina Bikira Mambisa msimamizi wa kisiwa cha Cuba. Tarehe 8 Septemba 1927 Madhabahu ya Bikira Maria wa Upendo  likatabarukiwa. 7 Juni -2 Septemba 1935 yalianzishwa mahusinao ya kidplomasia ya Vatican na Jamhuri ya Cuba. Tarehe 3 Septemba 1935, Vatican ikaweka makazi ya ubalozi wake kwa  kumteua Balozi wa kitume Monsinyo Giorgio Giuseppe Caruana ambaye tayari alikuwa huko tangu mwaka 1925 kama mwakilishi wa kitume .

Tarehe 20 Desemba mwaka 1936 Bikira Maria wa Cobre akawekea taji lake.Tarehe 28-29 Novemba 1959 ilifanyika Mkutano wa  kitaifa katoliki wa kwanza na Mkutano Mkuu wa Kitume Katoliki ulio itishwa na Maaskofu wa Cuba huko Avana. Kati ya matukio muhimu ni yale ya kuadhimisha misa katika Uwanja wa Mapinduzi wa Avan kwa ajili ya kutoa sifa ya Mama Maria wa upendo wa Cobre. Washiriki wa misa hiyo, Baba Mtakatifu Yohane XXII aliwatumia ujumbe kwa njia ya Radio katika  lugha ya kihispania,pia ujumbe huo ulikuwa unawalenga hata wanasiasa wa Kisiwa hicho.Alitoa wito kwa wakatoliki wa kisiwa cha Cuba kuwa mstari wa mbele katika ujenzi wa jamii inayosimamia urafiki,Kuheshimiana,  msamaha bila ubaguzi na mapatano ambayo yanajengwa kila siku ili kushinda ubinafsi na kutokuwa na maelewano. Aliwaomba wakae kidete katika kuimarisha amani ya kikristo na kuendeleza mshikamano wa tamaduni ya wakatoliki wa cuba.

28 Oktoba  2007 alitangazwa mwenye heri José López Piteira mjini Vatican ambaye  alikuwa ni mtawa na shemasi wa Shirika la Mtakatifu Agostino mzaliwa wa Cuba shahidi wa imani  kati ya mwaka (1912-1936). Julai 2011 wawakilishi wa Vijana wa Cuba wakisindikizwa na Kard Jaime Ortega Alamino waliudhuria kwa mara ya kwanza  Siku ya Vijana duniani huko Madrid Huispania. Mwaka 2012 Baba Mtakatifu Benedikto XVI alifanya Ziara ya kitume katika tukio la kuadhimisha miaka 400 ya hupatika kwa sanamu ya Mama Bikira Maria wa upendo wa Cobre. Wakati wa Ziara yake ya kitume Baba Mtakatifu Benedikto XVI alikutana na kuongea na  Fidel Castro na kukutana mara nne na Rais Raul Castro mfuasi  wa  kaka yake 2008. 

Mwaka 2012   Serikali ya Cuba ilitoa sheria ya  kufanya sikukuu ya Jumaa Kuu kufuatia maombi ya Baba Mtakatifu Benedikto XVI wakati wa ziara yake.Na baada ya miaka miaka miwili yaani 2014, ikakubaliwa kuwa siku ya kiaifa katika katiba ya nchi, ambapo Aprili 2014 kwa mara ya kwanza njia ya msalaba ikaoneshwa moja kwa moja kupitia vyombo vya habari. Kanisa la Cuba limeweka mpango wa kitume kuanzia 2014-2020 ,ikiwa na kauli mbiu ya "njia ya Emau".Mpango huo unahusu kuingizwa kwa ukristo katika ufunguo wa utume watu wanao anza njia mpya ya imani wakati wanaishi na mwalimu wao Kristo.

Aidha Mpango huo unajikita zaidi katika kutoa nafasi kuanzia  familia na jumuiya ya kikristo ambazo zinaalikwa kuendelea na mchakato wa uongofu ili kushuhudia maana  ya kuishi kikristo katika mazingira na wote kuwa mstari wa mbele. Tarehe 10 Mei 2015 Baba Mtakatifu Francisko alikutana mjini Vatican na Raul Castro.Ziara yake Rais Castro ilikuwa ni  kumshukuru Baba Mtakatifu  kwa juhudi za kutaka kuleta mahusiano ua nchi hiyo kati ya Avana na Marekani. Kuanzia tarehe 19 -22 Septemba 2015 Baba Mtakatifu Francisko alifanya Ziara yake ya kitume katika Bara la marekani  ambapo kwanza alipitia Cuba na baadaye kuendelea ziara yake ili kuudhuria mkutano wa dunia juu ya  familia huko Philadelfia. Ziara ya Baba Mtakatifu nchini Cuba ilikuwa na kauli mbiu " mmisionari wa Huruma".
Ikumbukwe kwamba mwaka 1998 Mtakatifu Yohane Paulo II alikuwa ametembelea kisiwa hicho akiwa mjumbe wa ukweli na matumaini, na Baba Mtakatifu Mstaafu benedikto XVI alifika huko kama muhujaji wa upend,  katika tukio hili Serikali ilitoa msamaha wa wafungwa 3,522.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.