2017-05-04 16:23:00

Baba Mtakatifu: Msiogope mfumo mpya wa mawasiliano Vatican!


Furaha yangu kubwa kuwakaribisheni katika tukio la mkutano wa kwanza wa mwaka wa Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican  ambayo inawajibisha kutafakari kwa kina fahamu za pamoja na kuchunguza  hatua gani zimepigwa na Baraza hili ambalo nilitaka kufanya mfumo mpya wa mawasiliano ya Vatican  na zaidi ya kutafakari juu ya mada za wakati  huu ambazo ni muhimu hasa kwa upande wa utamaduni wa digitali. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyoanza nayo wakati wa kutoa hotuba yake kwa  washiriki wa Mkutano wa Mwaka wa Sekretarieti ya mawasiliano Vatican Alhamis 4 Aprili, wakati mkutano huo ulianza tarehe tatu aprili 2017. Baba Mtakatifu Francisko anasema, mada kuhusu Mkutano wa mwaka wa Baraza la Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican ni mada ambayo iko ndani ya moyo wangu ,kwasababu nimesha gusia mara nyingi katika hotuba za matukio tofauti. Hiyo inawajibisha kugundua mbinu na mitindo mipya ya kutangaza Injili ya huruma kwa watu wote, katika mioyo ya tamaduni tofauti, kwa njia ya mitandao ambayo kwa mantiki ya utamaduni wa digital inaweka mbele yetu wakati huu.

Baraza ili ambalo linahitimisha miaka miwili  tarehe 27 Juni 2017 tangu kuanza kwake inawakilisha mabadiliko ya dhati katika kipindi cha  halisi na mpya ambayo inaendelea na mwendo kasi. Anaongeza akitoa mfano kwamba  , mishumaa miwili inajionesha katika muundo kamili . Hakuna haja ya kuogopa maneno haya . Muundo  mpya  siyo kupaka rangi vitu bali kutaka kutoa muundo wa mambo  yaani kuyaandaa kwa namna nyingine. Hiyo ni kazi ya kufanya kwa akili, unyenyekevu , na hata kwa nguvu lakini nguvu ya wema  ili kuweza kuunda mambo katika mundo kamili. Kwa njia hiyo, siyo baraza kutangaza mabaraza yaliyopita bali ni katika ujenzi wa taasisi mpya ya kweli kutoka ile ya zamani kama inavyoeleza katiba yake kwamba, mawasiliano ya sasa  yenye sifa ya uwepo wa maendeleo ya vyombo vya habari vya digital pia sababu ya maelewano ya pamoja  inahitaji kufikiriwa mfumo wa habari za Vatican , kuwajibika kuandaa mipango mipya ambayo inatoa thamani yake katika historia inayozidi kukuza  mawasiliano na kuendelea kutoa uamuzi wa na kushirikisha katika umoja wa uendeshaji.

Mfumo huo wa mawasiliano umetokana na mahitaji ya kile kinachojulikana  "kuunganisha digitali. Kwa dhati Baba Mtakatifu Francisko anasema nyakati zilizopita kila aina ya mawasiliano ilikuwa na mkondo wake mwenyewe. Kila aina ya usemi ilikuwa na mwakilishi wa kati mwenyewe, kwa mfano maneno yaliyo andikwa katika gazeti, au vitabu , picha na hata sinema  na televisheni, maneno, muziki nakanda . Aina zote hizi za mawasiliano leo hii zinatolewa katika sehemu moja na  kuchukua faida ya mfumo mmoja kama wa njia ya  leli. Kwa njia hiyo hata Gazeti la  L'Osservatore Romano kuanzia mwaka kesho wataingia kufanya sehemu ya Sekretarieti ya mawasiliano Vatican. Itawabidi watafute njia mpya na mang’amuzi  ya kuweza kufikia idadi kubwa wasomaji kwa njia ya mitandoa kuliko magazeti ya karatasi yaliyokuwa yanatumia hawali.
Hata Radio Vatican kwa miaka mingi imekuwa na mtindo wa aina yake ya  mawasiliano ambayo kwa sasa ni lazima kuzingatiwa  mfumo mpya kwa kutumia teknolojia ya kisasa na mahitaji ya nyakati za sasa.

Kwa namna hiyo Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza juu ya juhudi za Baraza la mawasiliano inavyojikita katika uendeshaji wa habari hasa katika nchi zenye uduni wa kiteknolojia , akifikiria bara la Afrika  katika masafa mafupi, na kwamba anapenda kusisitiza  kuwa masafa mafupi  hayakusitishwa kamwe. Na miezi ya hivi karibuni hata maktaba ya Vatican pia kiwanda cha uchapaji vitabu Poliglotta Vaticana navyo vitaingia kufanya sehemu moja ya jumuiya kubwa ya kazi   Baraza hili. Hiyo inahitaji uwezekano na ushirikiano ili kuoanisha  uzalishaji na ugawaji mpya.Kazi ni kubwa na changamoto ni kubwa lakini inawezekana na ni lazima Baba Mtakatifu amesisitiza. Bilashaka historia  hii Baba Mtakatifu Francisko anaendelea ni mali ya uzoefu wa thamani ya kutunza na kutumia ikiwa kama gurudumu la msukumo wa siku zijazo. Vinginevyo inaweza kupunguza uzuri kama wa jumba la makumbusho la kutembelea , lakini lisilokuwa na uwezo wa kutoa nguvu na ujasiri kwa ajili ya kuendelea na safari hiyo. Katika upeo wa ujenzi wa mfumo mmoja wa mawasiliano, Baba Mtaktifu anasema, ni lazima kuweka jitihada za mafunzo ya kudumu binafsi  na pia kwa wafanyakazi.

Aidha amesema kazi inayo wasubiri ni kubwa na nyeti. Kwa mchango wa kila mmoja ili kuweza kufikia ukamilifu wa mageuzi katika kutoa thamani ya historia imeweza kutoa maendeleo ndani ya mawasiliano ya Vatican na kushirikisha katika umoja wa uendeshaji. Anawatia moyo ili wafanya kazi katika kamati yao ya  mafunzo na kutathimini , kwani baada ya ugunduzi wa njia ya kufuata ,itawasaidia kutumia na kuendelea kwa ujasiri kwa mjibu wa mantiki iliyochaguliwa. Anawaomba zaidi ya mantiki hi iwaongoze ile ya  kitume, ya umisionari, zaidi kwa ajili ya hali za umaskini, wenye matatizo pia kuwa na utambuzi zaidi ili kupata mbinu za kukabiliana na hali hiyo.Kwa maana hiyo amewataka wapeleke Injili kwa  wote na kutoa thamani ya rasilimali ya binadamu bila kubadilisha mawasiliano ya Kanisa mahalia, wakati huo wakisaidia jumuiya ya Kanisa lenye kuwa na mahitaji. Baba Mtakatifu Francisko anatoa wito wa kupokea  mabadiliko kwani anasema;tusishindwa na kishawishi cha kushikiria sana mambo yaliyopita; badala yake ni kutengeneza kikundi kama cha wanamichezo wa pamoja ili kuweza kujibu changamoto za mawasiliano katika utamaduni wa leo ambao unao uliza, aidha kufanya hivyo bila hofu  na bila kufikiria matukio ya mwisho wa dunia. 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.