Ni karibu muhongo mmoja inaadhimishwa Siku ya Chuo Kikuu Katoliki. Ni mojawapo
ya tukio katika kalenda ya kila mwaka kwa wakatoliki nchini Italia, kufanya kumbukumbu
hii. Siku ya chuo Kikuu Katoliki imeandaliwa na Chuo Kikuu Katoliki cha Toniolo Milano
mbapo ni fursa ya kujikita kwa ndani katazama malengo ya Chuo Kikikuu katika msingi
na thamani yake inayo waongoza katika kufanya uchaguzi wa kila siku.
Katika kilele cha maadhimisho ya 93 ambayo yamefanyoka Jumapili tarehe 30 Aprili 2017,
ikiwa na kauli mbiu “kujifunza ulimwengu ambao umekwisha badilika”, Kardinali Pietro
Parolin Katibu Mkuu wa Vatican, ametuma ujumbe wake kwa Rais wa Chuo Kikuu Katoliki
cha Milano ambaye ni Kardinali Angelo Scola, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Milano na
kusema kuwa uwajibikaji wa mafunzo ya elimu ya juu malengo yake ya mwisho yasiwe
ya ubinasi, bali uwe ndiyo msukumo wa kwenda katika upeo wa nje.
Ni vema kwamba manufaa ya kuhitimu yawe ndiyo hisia binafsi inayowaongoza vijana katika njia ya kuendelea na masomo ya juuu ambayo yanakuwa makamilifu kwa upeo wa juukwa ajili yao binafsi, wengine na hata katika dunia.Kwa namna hiyo shuhuku ya haki , ukweli , uzuri uweze kutawanywa katika kila moyo wa binadamu ili kumsukuma katika mabadiliko, ya ujenzi wa majibu kwa ajili ya ulimwengu wa haki na kweli kutokana na kukomaa katika njia hiyo ya akili ya binadamu kwa miaka ya mafunzo ya chuo kikuu. Matukio mengi sana yanatoa msukumo kutazama kwa upya na hasa kuzingatia vijana.Kwa upande wao ,kuna umuhimu wa kutafakari pamoja kutokana na thari na wasiwasi mkubwa wa kiuchumi na kijamii kwa nyakati zetu,unaoleta kwa upande mwingine mahangaiko fulani ya kiroho. Wasiwasi wa kutokuwa na uhakika wa maisha endelevu na zaidi ukosefu wa ajira,suala la uhamiajai, matatizo yanayo kabiliana nayo katika kuingia maisha ya jamii hasa uhalisia wa kupanga mikakati ya kuunda maisha ya familia,ni changamoto inayobaki tete zaidi katika vizazi endelevu.Lakini pamoja na vipengele hivi muhimu, vijana wanabaki na matumaini makubwa kwa nguvu ya uzoefu kwa ajili ya kujenga maisha bora ya baadaye.
Pamoja na hayo yote mkono wa Yesu unaendelea kuwalinda na pia kuwatazama kwa matumaani, ukarimu ,kwa njia ya Kanisa kutokana na kuendelea na mipango ya kitume na mafunzo. Uwajibikaji huo unajikita zaidi hasa katika maamuzi ya Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya kukabiliana na Sinodi ijayo ya Maaskofu yenye mada ya Vijana. Imani na Mang’amuzi ya miito. Mpango wa Sinodi ni kutoka kuonesha kwa dhati ukaribu na upendo wa binadamu wote kwa ujumla wa Kanisa kwa kizazi endelevu, wakati huo huo ni kutaka kugundua kwa pamoja na vijana ili wao wawe mstari wa mbele katika maisha ya Kanisa na Jamii. Katika kuwajulisha vijana umuhimu wa matukio ya Kanisa, Baba Mtakatifu Francisko anawaalika kutafakari kwa kina imani ya Ibrahimu katika nyakati zetu,kwani yeye anatusukuma kwenda katika ardhi mpya ( Taz. Barua kwa Vijana 13 Januari2017). Baba Mtakatifu Francisko anawauliza vijana, je ardhi ni ipi kama siyo jamii ya haki na undugu ambao ninyi mnapenda kwa kina kuijenga hadi miisho ya dunia?
Pamoja na hayo yote vijana wanayo shahuku ya nguvu ya kwamba wasibaki watazamaji hivyo Baba Mtakatifu anawaalika wasizuie kilio chao cha dhamiri kitokacho ndani ya mioyo kwasababu kijana hakubalini na manyanyaso,ukosefu wa haki,utamaduni wa kubagua, na hata kukobea katika utandawazi wa utofauti. Ni katika mang’amuzi makini yaweza kusaidia vijana kukabiliana na changamoto kubwa. Lakini mang’amuzi hayo yanahusu watu wote kwa nyanja zote za maisha, inahitaji kusindikizwa na viongozi kwa njia ya wahudumu wa kichungaji wa kawaida ndani ya jumuiya,vyama vya Kanisa hata katika taasisi zote zenye uwezo wa kuhakikisha uwepo wa sifa ya kisayansi katika mafunzo ya utamaduni na kiroho.
Katika eneo hili jukumu kubwa muhimu ni juu ya Chuo Kikuu Katoliki, ambacho kimekabidhiwa utume wa kuandaa vijana wenye kuwa na uwezo wa kukuza rasilimali zao kiakili, ukarimu wa moyo kwa nguvu ya Roho wa maisha yao kwenye njia ya maisha endelevu ya ubinadamu. Kwa njia hiyo Chuo Kikuu hicho bado kina majukumu ya kuchangia na kuendeleza kwa uamininfu na ubunifu wa mpango ulio anzishwa na Padre Agostino Gemelli na washiriki wake wa Chuo Kukuu Katoliki cha Italia ambacho kinazidi kuwa kiungo kikuu kwa vijana wote wenye hamu ya kutoa mchango kwa ajili ya jamii ya haki na iliyo wazi na mshikamano. Kwa namna hiyo ni kuwatia moyo katika shughuli za Jumuiya ya Kanisa ya Italia ili kuendelea kusaidia Taasisi kuu ya elimu ambayo mwaka 2017 imefikia maadhimisho ya 93 yenye kuwa na kauli mbiu “ kujifunza ulimwengu ambao umekwisha badilika, ili ipate kutoa fursa ya kutafakari juu ya kujifunza na mafunzo kwa ujumla ya binadamu ambayo yanatazama mabadiliko ili wote waweze kutoa mchango katika kujenzi wa dunia iliyo bora tunayoishi.
Hii ni hisia ya kina kwa maana ya masomo ya Chuo Kikuu pia kipindi cha masomo ni muhimu kwa utambuzi binafsi na jamii. "Katika mazingira yoyote, hasa katika vyuo vikuu".Aliyasema Baba Mtakatifu Francisko akizungumza hivi karibuni katika Chuo Kikuu mjini Roma Tre - kwamba ni muhimu kusoma na kukabiliana na mabadiliko haya ya enzi za sasa , kutafakari na pia kufanya mang’amuzi, yaani, bila ya kiitikadi, chuki, bila hofu au kutoroka." Mang’amuzi hayo yanasaidiwa na ukweli kwamba "chuo kikuu ni sehemu ya nafasi ya upendeleo ambayo inalea dhamiri katika kupambana dhidi ya mahitaji mema, ya kweli na mazuri, vilevile ukweli wake katika utata,” (Hotuba katika chuo kikuu Roma Tre 17 februari 2017).
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |