2017-04-27 16:11:00

Jukwaa la Familia: Hali mbaya ya maisha nchini Italia kuongezeka


Kwa Mujibu wa takwimu zilizotolewa, ni zaidi ya milioni tatu za familia ambao wanafanya jumla ya watu milioni saba wanaoishi katika hali ya ukosefu wa mahitaji nchini Italia; hali hii inajulikana ambayo. Ni maneno ya  Gifi De Palo,Rais wa Jukwaa ya Vyama vya Familia nchini Italia, akielezea jinsi ya hali ya maisha ya watu nchini Italia inavyozidi kuwa mbaya sana kila siku. Amesema kwamba, wanapokea simu  kila siku na barua pepe kutoka kwa watu ambao wanashindwa kupasha nyumba zao joto na wamekuwa na migogoro kutokana na gharama zinazoongezeka bila kutarajiwa au kwamba wanayo madeni ya malipo ya bili au kwa ajili ya nyumba za kupanga.

Hiyo ndiyo hali halisi zaidi ya nchi ya Italia inayo wakumba wazalendo wake.Aidha Rais wa Jukwaa la vyama vya Familia amesema, ni kwa miaka mingi sasa wanazidi kutoa maoni yao na malalamishi kuhusiana ongezeko kukubwa la dharura inayojionesha katika takwimu na kwamba haiwezekani kuendelea kufikiri katika misingi ya dharura tu,kwasababu kutokana na nguvu ya kusubiri mwaka baada ya mwaka inasababisha migogoro ya umaskini  kuzidi zaidi kiasi cha kushindwa kurejesha hali sawa ya jamii kwa siku zijazo.

Aidha Bwana De Palo amesema kuwa wamechoka  daima  kuendelea kuulizia mambo hayo hivyo ni lazima kuweka kipaumbele kwa nguvu zote za kisiasa; kwani bila mageuzi ya kodi nchini Italia ambayo inalenga familia, kwa miaka ijayo idadi kubwa ya mateso ya watu itakuwa mbaya zaidi.


Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.