2017-04-23 10:57:00

Ni ustaarabu usio na kizazi; lakini pia unafunga milango kwa wahamiaji


Mwanzilishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Andrea Riccardi mara baada ya kumpokea Baba Mtakatifu Francisko katika Kanisa Kuu,ametoa hotuba fupi na kusema; Mashahidi wanakumbusha kwamba wakristo hawashindi kwa nguvu ya silaha, fedha na  ridhaa bali ni kutokana na ujazo wa nguvu ya imani,upendo, unyenyekevu na huruma. Katika kipindi cha changamoto ya ghasia , vita na ugaidi  kuna haja ya kutafuta ushindi, lakini ushindi huo utatokana na imani na umoja.Kwa njia hiyo Ricardi ameongeza kusema , maombi ya kumbukumbu ya mashahidhi kwa siku hii ni kuambatanisha na sala kwa ajili ya kuandaa ziara ya Baba Mtakatifu kuelekea Misri mapema tarehe 28-29 Aprili 2017, ni nchi ya mashahdi lakini pia ya mazungumzo .

Mara baada ya mkesha wa sala ya kuwaombea Mashahidi wa Karne ya XX na XXI ,Baba Mtakatifu ametoa shukrani zake kwa wote kuudhuria katika mkesha huo  na kusema  “ukifikiria ukatili wa sasa unaondelea  kwa watu wengi na pia unyanyaswaji  wa watu wanao fika na mitumbwi na kubaki pale katika nchi ambazo zina ukarimu kama vile Italia, Ugiriki. Nchi hizo zinawapokea , japokuwa pia mikataba ya Kimataifa haiwaachi”.Baba Mtakatifu ametoa mfano akisema ;” kama nchi ya Italia ingeamua  kila kata kupokea wahamiaji wawili,nafasi ingepatikana kwa watu wote.”

Aidha amewakumbuka kwa namna  pekee ukarimu unao fanywa na visiwa vya Lampedusa na Sicilia, kama vile Lesvos , na kwamba mfano huo unaweza kuambukiza hata maeneo ya Kanda za Kaskazini mwa Ulaya Ameongeza kusema Baba Mtakatifu Francisko kwa masikitiko  ; “ ni kwamba ustaarabu wa Ulaya hauna watoto lakini pia tunawafungia milango wahamiaji wasiingie; na hivyo hiyo inaitwa kujiua.Tuombe”.

Baadaye Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kikundi cha wakimbizi walio pokelewa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio. Kati ya hao kijana mmoja mkimbizi  kutoka nchi ya Eritrea ametoa zawadi ya Kadi iliyochorwa sura za waathirika  baharini kutokana na janga la tarehe 3 Oktoba 2013.Halikadhalika Baba Mtakatifu Francisko amebariki sanamu ya mti wa kuchongwa inayo onesha njiwa iliyoko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Bartholomew kwa ajili ya kumbukumbu ya mashahidi wapya.


Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.