2017-04-22 17:16:00

Vyombo vya habari na digital ni tishu muhimu tunazama ndani yake!


"Hatuwezi kuacha mazungumzo na utamaduni wa wakati wetu, pamoja na mageuzi ya vyombo vya habari na haja ya kujifunza lugha mpya." Ni maneno ya hotuba ya Monsinyo Edoardo Viganò, Mwenyekiti wa Sektretarieti ya Mawasiliano Vatican aliyotoa katika Semina kwa Muungano wa Wakuu wa Mashirika ya kitawa nchini Italia wakiwa katika ya mafunzo  yenye mada ya mchanganyiko  wa vyombo vya habari na digital. Monsinyo Vigano amebainisha kuwa hata Kanisa ni warithi wa nyakati zilizopita,"kwani hata sisi tunahifadhi kama hazina ya thamani, lakini tunao wajibu wa sasa unaojikita katika changamoto ya baadaye ambayo inahitaji ubunifu.”

Baba Mtakatifu Francisko anawakaribisha wote kutafakari juu hali halisi ya vyombo vya habari, na kwamba siyo tena vyombo vya bandia ambayo vinaruhusu kufika mbali zaidi, bali ni tishu muhimu ambayo sisi wote tunazama,ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Kwa uwelewa huo Monsinyo Vigano anaongeza kusema   “tunalazimika kuelewa umuhimu wake na kutambua vema mafunzo na matumizi ya vyombo vya habari bila kuwa na hofu na hali ya kubobea ndani yake; bali kwa uhuru na utulivu kama chipukizi anayetaka kujua zaidi.”Pamoja na mapinduzi ya kiteknolojia,amesema kuwa kuna swali kwamba vyombo vya habari vinafanya nini?. Monsinyo Vigano amesema,"ni lazima kuelewa changamoto za kiutamaduni kwa jamii na Kanisa kwa upeo mpya wa mawasiliano". Wakati huo huo Baba Mtakatifu Francisko anatukumbusha kwamba siyo teknolojia ambayo huamua kama mawasiliano ni halisi au la, bali ni moyo wa mtu na uwezo wake wa kutumia vizuri njia yake au la. Kwa maana hiyo Monsinyo anatoa wito wa kazi inayo takiwa kufanya hasa mada ya elimu na taarifa ambayo, matumizi ya mawasiliano ya jamii, inavyotaka kutumia mbinu mpya ya  utekelezaji na lugha ya awali na kama ile mbinu mpya ya kusimulia.

Monsinyo Viganò aidha amekumbuka maneno ya Baba Mtakatifu Francisko, ambaye anaonya juu ya kutengwa kijamii kutokana na kuenea kwa mahusiano ya mitandoa ya kijamii ya sasa, na ambayo inaendelea kudhoofisha mahusiano ya kweli. Kwa njia hiyo anasema ndipo mada muhimu ya mafunzo katika nyanja hii inabidi kutolewa mkazo  ili kuweza kukomaa katika uwajibikaji  wa kukaa ndani  au uhusiano na dunia mpya ya mitandao ya kijamii. Wakristo wanaitwa kuwa "wananchi na siyo wageni wa mitandao ya kijamii" . Bila shaka ni kutazam mazingira na sifa ya uhakika kwani anasema ni lazima kuchagua nafasi ya kukaa katika vyombo vya habari na digital pia hata muda wa kukaa pamoja na wengine kujadiliana  kwa kusikiliza,au kukaa kimya ili kusikiliza uwepo na sauti ya Mungu.

Kwa namna hiyo hata vyombo vya habari na mitando ya kijamii inaweza kuwa furs ambayo mahusiano uzaliwa lakini vinahitaji zaidi ya yote umakini daima. Katika sehemu ya mwisho ya hotuba yake, Monsinyo Viganò  amesisitiza juu ya "kutofautisha  na kuunganisha". Amesema ,katika upeo wa macho ya vyombo vya habari na digital kwa matumizi yenye usalama na hatari. Amesisitiza juu ya kuwa na matumizi sahihi katika mitandao, na hivyo anatoa mwito kwa  wakuu wa mashirika nchini Italia kutia juhudi ya kufanya mafunzo yanayo toa fursa ya matumizi madhubuti ya baadaye,kwa kujihusha katika maamuzi na malengo.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.