2017-04-22 19:09:00

Kuna wafiadini wengi katika dunia hii waliofichika katika ukimya !


Jumamosi tarehe 22 Aprili 2017 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Bartholomew Roma,Baba Mtakatifu Francisko ameadhimisha Liturujia ya Neno kwa ajili ya kumbukumbu ya mashahidi wa Karne ya XX na XXI akiwa na jumuiya ya Mtakatifu Egidio.Katika mahubiri yake Baba Mtakatifu Francisko amesema, kuwa wamefika kama mahujaji katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Bartolomeo kwenye Kisiwa Kidogo Tiberina, mahali ambapo historia ya zamani ya mashahidi inaunganisha na kumbukumbu ya mashahidi wapya, ambao ni wakristo wengi walio uwawa kwasababu ya itikadi za kiajabu kwenye muhongo ulio pita; lakini hata leo hii kuwawa kwasababu ya kuwa mitume wa KristoKumbukukumbu ya mashujaa wa kizamani ni  udhibitisho uliowazi wa utambuzi kwamba Kanisa ni Kanisa; na  kama ni Kanisa ni la kishahidi.

Baba Mtakatifu Francisko amesema  mashahidi wanaelezwa katika kitabu cha ufunuo kukumbusha  kwamba “Hawa ni wale waliopita salama katika ule udhalimu mkuu. Waliyaosha mavazi yao katika damu ya mwanakondoo yakawa meupe kabisa "(Uf 7,14).Baba Mtakatifu amesema, wao walipata neema ya kuamini Yesu hadi mwisho  wa mauti yao.Wao waliteswa na wanatoa maisha na kwa njia hiyo sisi tunapokea baraka  za Mungu kwa njia ya ushuhuda wao. Kuna hata mashahidi ambao wamefichika, hawa ni wanawake na wanaume waaminifu, wanyenyekevu wa upendo,kwa  sauti ya Roho Mtakatifu ambao kila siku ya maisha yao wanajikita kusaidia ndugu , na wanampenda Mungu bila kubakiza.

Iwapo tunatazama vizuri,sababu ya kila mteswa, ni kwa njia ya chuki: chuki ni mfalme wa ulimwengu huu dhidi ya walio kombolewa na Yesu kwa njia ya kifo na ufufuko wake. Katika Injili ya Yohane ,Yesu ametumia neno la kuogopesha, yaani chuki.  Yesu ni mwalimu wa upendo ambaye daima alipendelea kuongea juu ya upendo na pia chuki. Lakini daima alipendelea kuita kila kitu kwa jina,ndiyo maana anawambia mitume wake  msiogope maana dunia itawachukia, lakini kabla yenu ilinichukia mimi.( Yh 15,12-19).Yesu alituchagua kwa zawadi ya bure ya upendo wake. Kwa njia ya kifo na ufufuko wake ametukomboa dhidi ya utawala wa dunia hii, ni utawala wa ibilisi, utawala wa mfalme wa dunia hii. Na chanzo cha chuki ndiyo hiki, kwasababu sisi tumekombolewa na Yesu, ambapo  mfalme wa duna hii hapendi jambo hili, yeyé anachukizwa na ndiyo maana anatengeneza watesi ambao tangu wakati wa Yesu yaani tangu Kanisa kuanza  hadi kufikia nyakati zetu. Kwa njia ya mateso hayo ;Baba Mtakatifu Francisko ametoa mfano akisema, ni jumuiya ngapi za Kikristo leo hii wanakabiliwa na mateso !Je, ni  kwa nini? Ni kwa sababu ya chuki ya roho ya ulimwengu huu.

Aidha amasema mfano mwingine “ ni mara ngapi katika kipindi kigumu, unasikia wanasema, "leo hii nchi inahitaji washujaa". Kwa namna hiyo shahidi anaweza kufikiriwa kama shujaa, lakini msingi wa ushujaa alio pata ni kutokana na neema ya Mungu na siyo ujasiri unaofanywa na shahidi yeye binafsi.
Hata leo unaweza kuuliza Kanisa linahitaji nini? anesena Baba Mtakatifu kwamba Kanisa leo hii linahitaji mashahidi, mashuhuda , yaani utakatifu wa kila siku kwasababu Kanisa daima wapo watakatifu mbel ambapo bila  wao Kanisa haliwezi kwenda mbele.Kanisa linahitaji watakafiu kila siku,wanaoishi maisha ya kawaida, ambao wanapeleka ushuhuda huo kwa udhabiti; lakini pia wale walio na ujasiri wa kukubali neema kuwa mashihidi hadi mwisho wa kifo. Hawa wote ni damu hai ya maisha ya Kanisa. Ni mashahidi wanao endeleza mbela Kanisa , wale wanao dhibitisha kwamba Yesu amefufuka na Yesu yuko hai, kushuhuda kwa uadilifu wa maisha na Roho Mtakatifu waliyokwisha pokea kama zawadi.

Baba Mtakatifu pia ameongeza kwamba, angependelea kuongeza picha zaidi katika Kanisa hilo, mwanamke mmoja na hajuhi jina lake, japokuwa amesema kwamba,yeye anatutazama akiwa mbinguni.Amesimulia  kuwa, alivyo kuwa kwenye ziara yake huko Lesbos akisalimiana na wakimbizi , alikutana na mwanaume mmoja wa miaka 30 hivi na watoto watatu. Alimtazama na kusema; Baba mimi ni mwislam:Mke wangu alikuwa mkristo.Na katika nchi yetu walifika magaidi na kuulizia dhehebu gani, ambapo mke wake alikuwa na msalaba shingoni , walimwomba autupe chini. Na yeye hakufanya hivyo ndipo akakatwa shingo lake mbele ya mme huyo. Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema “mwanaume huyo alisema jinsi walivyokuwa wakipendana sana. 

Katika historia hiyo fupi, Baba Mtakatifu Francisko amesema ndiyo picha anayo toa kama zawadi katika Kanisa kuu hilo. Akaongeza ; hajuhi kama yule mwanaume bado yuko  Lesvos  au kama  amefanikiwa kwenda mahali pengine. Na hajuhi kama ameweza kufanikiwa kutoka katika mkusanyiko wa umati wa makambi ya wakimbizi.Ameongeza;”Watu wakarimu wanao pokea wakimbizi hao wanalazimika kubeba uzito huo kwa sababu inaonekana kwamba mikataba ya kimataifa ni muhimu zaidi kuliko haki za binadamu. Na mtu huyu hakuwa na kinyongo japokuwa alikuwa mwislam na kuchukua msalaba wa uchungu mbele bila kuwa na kinyongo .Alichukua hifadhi katika upendo wa mke wake, aliyeteswa kama shahidi”.

Baba Mtakatifu Francisko amemalizia mahubiri yake akisema;kukumbuka mashihidi hawa wa imani na kusali katika eneo hilo ni zawadi.Ni zawadi ya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio,kwa ajili ya Kanisa la Roma na kwa ajili ya jumuiya za Kikristo katika mji na pia kwa mahujaji wote.
Urithi hai wa mshahidi wa leo unatupatia imani na umoja.Unatufundisha kwamba kwa nguvu ya upendo na upole tunaweza kupambana dhidi ya uonevu,vita, na tunaweza kwa kuwa wavumilvu ili kufikia amani.Kwa njia hiyo tunaweza kusali : Ee Bwana tufanye tuwe mashahidi wa Injili wanaostahili , wa upendo wako, utupe huruma yako juu ya ubinadamu,ufanye upya Kanisa lako na uwalinde wakristo wanaoteseka na mwisho utupatie haraka amani duniani.

Sr Angela Rwezaula

Udhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican. 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.