Timu ya wanamichezo wa Vatican (St Petr’s Cricket Club) iliyoazishwa Oktoba 2013
na Baraza la Kipapa la Utamaduni litakwenda kupambana na timu michezo za umoja wa
makanisa kwa ajili ya mazungumzo ya kiekumeni Ureno.
Timu hii ilianzishwa kwa mawazo ya Balozi wa Australia aliyeko katika Ubalozini
Vatican, John McCarthy kwa lengo la kujenga madaraja ya dini na utamaduni, kwa njia
ya michezo. Katika timu ya Vatican washiriki wa timu hiyo ni Mapdre, mashemasi na
waseminari kutoka nchi ya India, Pakistan, na waingereza wanaosoma katika vyuo mbalimbali
vya kipapa Roma.
Mashindano ya mwaka huu wameamua kwenda kuchezea nchinii Ureno, kutokana na tukio la miaka 100 ya kutokea Mama Maria huko Fatima. Wachezaji watakabiliana na wanamichezo kutoka nchini Ureno Hispania na Uingereza , wakiwa ni mchanganyiko wa dini tofauti , wakiwemo waislam , wayahudu na wahindu.Siku ya kwanza watazunguka na kutembelea Kanisa Kuu la Mama Maria wa Fatima. Mashindano ya mchezo wa kwanza uli fanyika Septemba 2014 , kabla ya tukio hili kuanza safari kuelekea Uingereza, Baba Mtakatifu Francisko alikutana katika mkutano binafsi tarehe 9 Septemba 2014.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahi ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |